Mlipuko mkubwa umetokea mjini Lagos

Mlipuko mkubwa umetokea mjini Lagos

Mlipuko mjini Lagos
Mlipuko mkubwa umetokea mjini Lagos
Maafisa wa kuzima moto wakiendelea na kuzima moto katika ghala moja lililolipuka Lagos

Moto mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Nigeria Lagos.
Taarifa zinaarifu kuwa moto huo ulianza katika eneo la kuhifadhi baruti na kisha kuenea kwa haraka katika majengo mengine yaliyo karibu na ghala hilo.
Moshi mkubwa umeenea kote katika kisiwa cha Lagos na wazima moto wanajithidi kuuzima moto huo.
Bado baadhi yamajengo yanaendelea kuteketea.
Mwandishi wa BBC anasema maafisa wa kuzima moto walikuwa na wakati mgumu kufika eneo hilo kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa hapa.
Kwingineko, maafisa wa usalama Kaskazini mwa Nigeria wanasema watu waliojihami kwa bunduki wamefyetua risasi na kuwaua watu sita katika kijiji chenye idadi kubwa ya wakristo.
Msemaji wa jeshi ameiambia BBC, kuwa washambuliaji hao waliwafyetua risasi waumini katika kanisa dogo wakati wa ibada ya Krismasi.
Mshambuliaji mmoja amezuiliwa na maafisa wa usalama katika eneo hilo.
Ripoti zaidi zinasema kuwa ulinzi umeimarishwa ili kuwaondoshea wasiwasi wakaazi wa eneo hilo.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo katika jimbo la Yobe, lakini kundi lenye itikadi kali za dini ya Kiislamu la Boko Haram limekuwa likiwalenga Wakristo katika eneo hilo mara kwa mara.
Share this product :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger