Friday, December 14, 2012

KOFFI OLOMIDE AWASILI DAR KUWARUSHA MASHABIKI WA SEBENE JUMAMOSI LEADERS CLUB


Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi kutoka DRC-Kongo, Koffi Olomide, akipunga mkono kusalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana usiku  wakati akiwasili pamoja na kundi lake zima la Quartier Latin,kwa ajili ya onesho lake litakalofanyika kesho siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba. Onesho hilo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker na kiingilio katika shoo hiyo kitakuwa ni sh. 10,000/= kwa mtu mmoja na kwa wale watakaokatia tiketi mlangoni watalipia sh. 15,000/= getini. Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga


  Baadhi ya wanamuziki wa Koffi Olomide wakishuka kwenye gari kwenye viunga vya hoteli ya Serena usiku wa kuamkia leo .


Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About