Friday, January 4, 2013

Mkuu wa polisi atekwa nyara LibyaMaafisa wa polisi wa Libya wakikabithiwa silaha

Watu wenye silaha wamemteka Kaimu Mkuu wa Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai wa mji wa Benghazi, ambao wa pili kwa ukubwa nchini Libya.
Abdelsalam al-Mahdawi, ametekwa akiwa barabarani kwenye taa za barabarani, alipokuwa akielekea kazini.
Hadi sasa bado haijulikani ni kundi lipi lilihusika na shumbulio hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani Ashour Shwayel, ameahidi kumsaka afisa huyo wa polisi, pamoja na wahalifu waliohusika na utekaji huo.
Mamlaka nchini Libya, imekuwa ikiimarisha ulinzi tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddaf mwaka 2011.
Mwezi Novemba, mwaka uliopita mkuu wa polisi wa Beghazi, aliuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akiendesha gari.
Idadi kadhaa ya maafisa usalama wameuawa katika mji wa Benghazi, ambao ndio mahali mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Muammar Gadaffi.

Maafisa wa polisi walengwa na wahalifu

Shirika la habari la AFP, limemnukuu Afisa moja wa usalama akisema kwamba Afisa huyo wa upelelezi alikuwa na maadui wengi.
"Alikuwa akifanya kazi inayowagusa karibu kila mmoja, Wanaomuunga mkono Gaddafi, Waislamu wenye msimamo mkali na wahalifu," Amesema afisa huyo ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Shambulio katika Ubalozi wa Marekani mjini Benghazi
Kundi la maafisa wa polisi wameandamana kupinga utekaji nyara huo.
Mmoja kati maafisa hao alikuwa na bango linauliza "Wako wapi wanaume wa Benghazi?"
Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya mashambulizi kwenye ofisi za ubalozi na mashirika ya misaada katika mji huo wa Benghazi.
Moja kati ya matukio hayo ni la mauaji ya Balozi wa Marekani, yaliyotokea mwezi Septemba mwaka uliopita.
Vile vile kumekuwa na matukio ya mashambulizi kwenye majengo ya ibada ya Sufi pamoja na Misikiti.
Mashuhuda wanasema mashumbulizi hayo yamekuwa yakitekelezwa na wanamgambo wa ya Kiislamu.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About