Thursday, January 3, 2013

Watu 20 wafariki kwenye ajali Kenya

Matatu iliyohusika kwenye ajali hiyo

Takriban watu ishirini wamefariki kwenye ajali mbaya ya barabarani nchini Kenya, baada ya gari moja ya abiria maarufu kama matatu, kukosa mwelekeo na kutumbukia ndani ya chimbo la mawe.
Ripoti zinasema watu wengine saba wako katika hali mahututi.
Gari hilo ambalo linaruhusiwa kubeba abiria kumi na wanne pekee inasemekana kubeba zaidi ya abiria 28.
Ajali hiyo ilitokea magharibi mwa nchi hiyo ambako barabara ni mbovu na inatokea siku moja tu baada ya watu wengine kumi na moja kufariki katika eneo hilo hilo.
Idara ya polisi nchini humo imeanzisha uchunguzi kufuatia ajali hiyo.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo amesema, maafisa wa polisi watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa itabainika kuwa gari hilo lilipita katika kituo chochote cha ukaguzi na hakiku kamatwa kwa kubeba abiria kupita kiasi.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About