Welcome to our online store Portal

Template Information

Wednesday, January 23, 2013

Watu 5 wakatwa vichwa Maiduguri,Nigeria


Washukiwa wa kundi la kiisilamu wamewakata vichwa watu kadhaa mjini Maiduguri, Kaskazini mwa Nigeria.
Mtu mmoja ameambia azizicompdoc.blogspot.com  kuwa wanaume watano waliuawa wakati wa msako katika nyumba za watu usiku wa kuamkia leo.
Miongoni mwa walionyongwa ni baba na mwanawe.
Hata hivyo, jeshi la Nigerialimesema ni watu watatu pekee waliouawa.
Zaidi ya watu 20 sasa wamefariki katika mashambulizi tofauti, Kaskazini mwa Nigeria wiki hii pekee ambayo yanshukliwa kusababishwa na kundi la
Boko Haram pamoja na makundi mengine yanayotaka nchi hiyo kutumia sheria za kiisilamu.
Boko Haram wamelaumiwa kwa mauaji ya watu 23 katika mashambulizi tofauti Kaskazini mwa Nigeria.
Walio shuhudia mauaji hayo wanasema kuwa washambuliaji waliwalenga watu waliokuwa wanauza nyama ya wanyamapori, katika eneo la Damboa siku ya Jumatatu na kuwaua watu 18.
Watu wengine watano walifariki Jumanne wakati kundi la wanaume waliokuwa wanacheza mchezo wa kamari walishambuliwa mjini Kano.
Kundi la Boko Haram, linalopigana kutaka kuweka sheria za kiisilamu, nchini Nigeria limekuwa likifanya mashambulizi, katika sehemu kadhaa nchini humo.
Boko Haram imelaumiwa kwa vifo vya takriban watu 1,400, Kaskazini mwa Nigeria tangu mwaka 2010. Mwaka jana pekee , kundi hilo lilihusishwa na vifo vya watu 600.
Siku ya Jumatatu, watu waliokuwa wamejihami, walifyatulia risasi katika soko moja jimbo la Borno , wakiwalenga watu waliokuwa wanauza nyama ya nyani, na nguruwe.
Silaha zilizonaswa kutoka kwa kundi la Boko Haram

Waisilamu wengi hawatumii kabisa nyama ya wanyama pori.
"watu waliokuwa wamejihami, na wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram, walikuja katika soko moja eneo hilo, na kuwapiga risasi watu 13, papo hapo na wengine watano walifariki kutokana na majereha yao.'' alisema afisaa mmoja.
Eneo la Damboa liko karibu na hospitali moja mjini Borno katika jimbo la Maiduguri, ngome ya Boko Haram.Kundi hilo liliundwa mjini humo mwaka 2002.
Wakati huohuo, ripoti zinasema kuwa shambulizi lengine baya sana limefanywa mjini Kano , mji mkuu Kaskazini mwa Nigeria,umbali wa kilomita 500, Magharibi mwa Damboa.
Watu waliokuwa wanaendesha pikipiki waliwanywaftulia risasi, vijana waliokuwa wanacheza nje , kwa mujibu wa taarifa za polisi.
Mchezo wa kamari pia umeharamishwa katika dini ya kiisilamu.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop