Welcome to our online store Portal

Template Information

Wednesday, January 23, 2013

Bi Clinton kujitetea kuhusu Benghazi


Bi Clinton alitarajiwa kuhojiwa mwaka jana lakini akaugua
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, anatarajiwa kufika mbele ya bunge la Congress kujieleza kuhusu mashambulizi mabaya yaliyofanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi, Libya, mwaka jana.
Bi Clinton atakabiliwa na maswali kutoka kwa kamati za bunge la Senate na la waakilishi kuhusu maswala ya kigeni, juu ya usalama mbovu uliosababisha mashambulizi hayo.
Alitarajiwa kujieleza mbele ya kamati hiyo mwaka jana lakini akaugua.
Balozi wa Marekani nchini Libya Christopher Stevens pamoja na maafisa wengine watatu wa ubalozi huo, waliuawa kwenye mashambulizi hayo.
Balozi huyo alifariki kutokana na moshi wakati aliponaswa ndani ya jengo lililokuwa linateketea.
Hii ni baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuvamia ubalozi.

Mashambulizi hayo yalisababisha mvutano wa kisiasa swali lilikuwa nani aliyekuwa na taarifa kuhusu shambulizi hilo.


Baada ya kushambulia ubalozi wavamizi walichoma bendera ya Marekani kuonyesha kero lao
Kutokana na hilo, jopo maalum lilbuniwa kuchunguza tukio hilo.
Kwa kuwa Clinton ni mwanachama wa Democrat ambao wanadhibiti bunge la Senate, atakuwa anahojiwa kwa njia ya heshima lakini atakabiliwa na wakati mgumu kutoka kwa wabunge wa bunge la waakilishi ambao wengi ni wanachama wa Republican.
Jopo hilo huenda lisimlimbikizie lawama sana Clinton kwa utovu wa usalama kwenye ubalozi huo, lakini wanachama wa Congress bado watataka kujua kwa nini hakuwa na taarifa kuhusu ombi la kuimarisha usalama katika ubalozi huo.
Pia atakabiliwa na maswali kuhusu ambavyo serikali ya Obama ilishughulikia mzozo huo.
Wafanyakazi watatu wa serikali walifutwa kazi kuhusiana na shambulizi la Benghazi na mapendekezo yaliyotolewa na jopo hilo mwezi Disemba tayari yanashughulikiwa.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop