Akizungumza na gazeti hili jana Katibu wa CCM
mkoani humo, Alhaji Masoud Mbengula alisema chama kilishangazwa na kauli
za mbunge huyo, kwa mba alionekana wazi kuwaunga mkono wapinzani na
siyo wananchi.
“Tayari tumemwita katika vikao na kumhoji
kuhusiana na kauli alizozitoa, pia taarifa rasmi zipo na tumezipeleka
makao makuu ya chama ambapo ndiyo watatoa uamuzi,” alisema Mbengula na
kuongeza;
“Tumesikitishwa sana na kauli ya Murji. Kauli yake
ilionekana kuwaunga mkono wapinzani kwa kuwa msimamo na nia yao ni
kuona Ilani ya CCM haitekelezwi. Kama alikuwa na hoja alitakiwa kutafuta
njia za kusema na siyo kuzungumza jambo hilo hadharani. Kwa namna moja
au nyingine yeye amechangia kukihujumu chama.”
Wakati katibu huyo akieleza hayo, Desemba 29 mwaka
jana baada ya Murji kutoonekana kwenye maandamano ya wakazi wa Mkoa wa
Mtwara ya kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam yaliyofanyika Desemba 27,
aliibuka na kusema anaunga mkono wananchi hao kutetea maslahi yao.
Alisema hoja ya msingi ni kujadili kwa namna gani bomba la gesi litanufaisha Wanamtwara, kufafanua kuwa kwa kiasi fulani hakubaliani na hoja ya gesi isiende Dar es Salaam lakini naungana na wananchi kudai jinsi watakavyonufaika na gesi hiyo.
Alisema anakubalina na gesi iende Dar es Salaam
kwa sharti la kuzalisha umeme, si kwa matumizi mengine, kwamba wakianza
kuitumia kwenye viwanda watakuwa wameiua Mtwara kabisa, huku akiunga
mkono wana nchi kuandamana kwa maaelezo kuwa ni haki yao ya msingi na
hawapaswi kubezwa na mtu yeyote kwa sababu wanateteta haki yao ya msingi
ya kufaidika na rasilimali yao.
Katika maelezo yake Mbengula alisema chama hicho
kilihujumiwa huku akitoa mfano wa matukio ya kuchoma moto nyumba. Nyumba
hizo nyingi zilikuwa za viongozi wa CCM wakiwamo wabunge pamoja na
ofisi, hasa zipo zilizochomwa wilayani Masasi mkoani humo.
“Nyumba zilizochomwa moto zote ni za viongozi na
wabunge wa CCM. Mpango huu ulionekana kupangwa na kuratibiwa na watu
fulani kwa lengo la kukihujumu chama” alisema Mbengula.
Murji
azizicompdoc.blogspot.com Jumapili jana lilizungumza na Murji ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa kauli alizozitoa nazo ziliungwa mkono na CCM.
azizicompdoc.blogspot.com Jumapili jana lilizungumza na Murji ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa kauli alizozitoa nazo ziliungwa mkono na CCM.
“Hata siku moja zikuwahi ku pinga gesi kwenda Dar
es Salaam.Lengo langu ni kutaka wananchi wafaidike kwanza na gesi, watu
walitaka kujua watanufaika vipi na si vinginevyo,” alisema Murji na
kuongeza;
“Hata katika ufafanuzi alioutoa Waziri Mkuu alieleza jambo hilo, hata CCM waliungana na mimi kutaka gesi iwanufaishe wakazi wa Mtwara.”
“Hata katika ufafanuzi alioutoa Waziri Mkuu alieleza jambo hilo, hata CCM waliungana na mimi kutaka gesi iwanufaishe wakazi wa Mtwara.”
Alisema kuwa kwa sasa hali imekuwa shwari mkoani
humo, huku akiwataka wananchi kuwa watulivu, kwani tayari Serikali
imeshaeleza msimamo wake na jinsi itakavyotekeleza mradi huo.
0 comments:
Post a Comment