Wananchi waliokua ktk eneo la tukio wakishuhudia moto huo
Maduka kadhaa ya vipodozi, nguo yameungua moto na kusababisha hasara kubwa kwa wamiliki wake.
Moto huo umetokea mishale ya saa 5.20 leo asubuhi baada ya kutokea hitilafu ya umeme kwenye moja ya kibanda cha biashara.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, moto huo ulianza taratibu kisha kupamba moto.
Wafanyabiashara wa maduka ya vipodozi ndiyo waliopata hasara kubwa kwa mali zao kuharibika kufuatia kutaka kuziokoa.
Hata hivyo, Kikosi cha Zima moto kilichofika eneo la tukio kwa wakati na kimepongezwa kwa kufanya kazi nzuri na kuweza kuudhibiti moto huo.
Aidha, jeshi la polisi limepongezwa kwa kazi nzuri lililoifanya ya kudhibiti vibaka ambao walijiandaa kufanya uhalifu wa kuiba mali katika kurupushani hizo za uokoaji.

Mabati yalivyoungua ktk baadhi ya maduka
Askari wa jeshi la polisi wakihakikisha usalama unaimarika ktk eneo la tukio, kuhakikisha mali za waathirika wa moto huo zinakua salama
0 comments:
Post a Comment