![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/05/130205124225_chad_soldiers_mali_304x171_reuters_nocredit.jpg)
Takriban wanajeshi 1800 kutoka
nchini Chad wameingia mji wa Kidal, Kaskazini mwa Mali ukiwa ndio mji wa
mwisho uliokuwa umetekwa na wapiganaji wa kiisilamu.
Wanajeshi wa Ufaransa waliuokomboa uwanja wa Kidal wiki jana ingawa bado hajaweza kukomboa mji wenyewe.Baada ya wapiganaji wa kiisilamu kutoroka, wapiganaji wa Tuareg wafanikiwa kuudhibiti mji huo tena.
Maafisa wa UN, EU na Afrika, wanakutana mjini Brussels kujadili namna watakavyofadhili na kupanga kuikarabati Mali.
Swali moja nyeti ni namna ya kuandaa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 31 mwezi Julai.
Waasi wa Tuareg hawakutaka jeshi la Mali linaloshirikiana na wanajeshi wa Ufaransa, kuingia Kidal baada ya kudai kuwa waliwaua raia wa Tuareg katika miji mingine ambayo wamefanikiwa kuikomboa.
Mkutano unaoendelea mjini Brussels umepatia maswala ya ukarabati , upatanishi na mchakato wa uchaguzi wa Mali kipaombele,
Lakini hii inaonekana kuhujumu kauli inayoonekana kutolewa na wananchi wengi wa Mali, kwamba hawataki upatanishi na kabila la wanaoishi Kaskazini mwa Mali.
Wanasema kuwa jamii ya Tuareg ni ya watu wachache sana wanaoishi Kaskazini.
Maafisa wengi nchini Mali wanataka tu kujenga upya jeshi lao ili waweze kudhibiti eneo la Kaskazini wala sio swala la upatanishi.
Jeshi la taifa linaoneakana kupata kipigo na sasa linatafuta kulipiza kisasi.
0 comments:
Post a Comment