Thursday, February 7, 2013

SHEREHE ZA KUADHIMISHA MIAKA 36 YA KUZALIWA KWA CCM MKOA WA LINDI ZATIKISA MJIViongozi wa CCM Wakiongozwa na Mama Salma Kikwete  wakikata keki kuashiria kuzaliwa kwa chama hicho

Mjumbe wa Halmashauri kuu wilaya ya Lindi ambae pia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewahimiza Wazazi mkoani Lindi kusimamia elimu ya watoto wao kwa kuhakikisha kuwa wanaenda shule ili kusaidia kuondokana na tatizo la watumishi waendeshaji na wanataaluma  katika mkoa huo ulio na rasilimali nyingi kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika kimkoa katika kata ya Chiponda -Rondo wilaya ya Lindi vijijini.
Mama Kikwete alipokua Lindi alieleza kuwa kutokana mikoa hiyo kuwa nyuma kimaendeleo sasa ifike wakati Wazazi na walezi kusaidia na kuakikisha watoto wao wanapata elimu kufuatia matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha pili hivyo basi kina baba washirikiane na wake zao kuhakikisha kuwa watoto wanahudhuria shule na kufanya vizuri katika masomo yao. 


Aidha Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM taifa aliwataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kutosubiri nafasi za upendeleo(viti maalum)
‘Wanawake wenzangu mjitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani na nje chama ili muingie katika ngazi ya maamuzi na kuachana na mawazo kuwa hamuwezi kuingia katika chaguzi za wananchi'alisema.
Sambamba na sherehe hizo Mama Kikwete aliwataka Wananchi wa Mkoa huo kuendelea kudumisha amani, upendo na utulivu, kufanya kazi kwa bidiii, maarifa na kujituma, wakulima walime kilimo cha kisasa ambacho kitawafanya wavune mazao mengi.

Awali Mama Kikwete pia alifungua jengo la ofisi ya CCM lenye thamani ya shilingi milioni 35 ambalo limejengwa na Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe.
Waziri Membe alisema kuwa jengo hilo lina vyumba sita ambavyo ni ofisi za jumuia zote za chama hicho ambazo ni Vijana, Wanawake, Wazazi, pia kuna ofisi za Mbunge, Mjumbe wa NEC na chumba cha mikutano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Ally Mtupa aliwataka wanachama wa chama hicho kuwa na mahusiano mazuri baina yao na viongozi wanaowaongoza. Wakisikia jambo wasiwe na papara ya kukimbilia kuandamana bali wafanye upelelezi kwanza na wakishabaini ukweli ndipo wachukue hatua. 

Mtupa alisema, “Hivi sasa kuna watu wanapita mitaani na kupotosha ukweli kuwa Serikaliyetu haijaleta maendeleo, wamesahau kuwa wanatembea katika barabara na kutibiwa katika Hospitali zilizojenga na CCM, tunawaomba watu hawa wawaheshimu viongozi wanaotawala kwani hata vitabu vya dini vinasisitiza umuhimu wa kuwatii viongozi waliopewa mamlaka ya kutawala”.
Sherehe hizo zilienda sambamba na mchango wa matembezi ya mshikamono ambapo zaidi ya shilingi milioni mbili zilipatikana, ufunguzi wa ofisi za CCM Kata ya Chiponda, ufanyaji wa usafi wa mazingira , kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, utoaji wa kadi kwa wanachama wapya ambapo wanachama wapya wa CCM 286 walijiunga,Jumuia ya wazazi 63 na kutoka vyama vya upinzani 23 walipewa kadi katika sherehe hizo.

Wanachama wa ccm wakisikiliza hotuba ya Mjumbe wa Nec,Mama salma kikwete

Mjumbe wa Nec,Mama Salma Kikwete akifurahia burdan iliyokuwa inatolewa na Wasanii katika sherehe za ccm


Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About