Friday, March 15, 2013

28% YA WANAFUNZI WAMEAMBUKIZWA HIV AFRICA YA KUSINI


wasichana waambukizwa Ukimwi nchini SA


Waziri wa afya wa Afrika Kusini Amesema kuwa zaidi ya asili mia 28% ya wasichana wa shule wameambukizwa virusi vya Ukimwi, ikilinganishwa na asili mia 4% tu ya vijana wa shule.
Hii ameelezea ni kutokana na kuongezeka kwa mababa sukari au kwa jina lingine, *fataki*, ( Wazee wanao tembea na wasichana wadogo kwa umri).
Waziri Aaron Motsoaledi amesema kuwa wamepata ushahidi kuwa wasichana wengi wamejiingiza katika mapenzi na wazee waliowazidi ki umri badala ya kuwa na vijana wa rika lao.


Madawa ya ARV

Takwimu za punde zaidi zimeonyesha kuwa asili mia kumi ya raia wa Afrika Kusini wanaishi na virusi vya HIV. Nchi hiyo imekuwa na mradi wa kuvuma zaidi wa kutoa dawa za kukabili makali ya virusi hivyo vya HIV , ARV tangu rais Jacob Zuma alipomteua bwana Motsoaledi kuongoza wizara hiyo ya afya yapata miaka minee iliyopita.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About