Welcome to our online store Portal

Template Information

Wednesday, March 13, 2013

MJI MUHIMU WA CAR WATEKWA NA WAASI

Waasi wa Seleka wauteka mji muhimu kusini mwa CAR 
 
Kundi moja la waasi katika Jamhuri ya Afrika ya kati CAR, limeuteka mji muhimu kusini mashariki mwa nchi hiyo karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Duru zimearifu kuwa Jeshi lilijiondoa kutoka mji wa Bangassou bila pingamizi yoyote. Kundi hilo la Seleka lilisaini mkataba na serikali mwanzoni mwa mwaka huu na likapewa uongozi wa baadhi ya wizara kuu za serikali. Hata hivyo tangu wakati huo limekuwa likilalamikia baadhi ya masuala linalodai kuwa hayajatatuliwa.

Seleka (jina hilo likimaanisha muunguano) liliteka miji mingi nchini humo na hata kutishia kuuteka mji mkuu Bangui. Walisaini mkataba na serikali mnamo Januari 11 katika mji mkuu wa Gabon Libreville chini ya utawala wa Francoise Bezize.
Mkataba huo ulifanikishwa kwa upatanishi wa viongozi wa eneo hilo na uliunda serikali ya muungano wa kitaifa na sasa inaongozwa na kiongozi wa upinzani Nicolas Tiangaye.
Tangu kuundwa serikali hiyo Seleka wamekuwa wakitilia shaka nia ya serikali na kuilaumu kwa kuendesha serikali mbadala inayohujumu nafasi yao. Wametishia kujiondoa kutoka serikalini mara kadhaa.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop