Welcome to our online store Portal

Template Information

Monday, May 20, 2013

VURUGU KUBWA ZAZUKA IRINGA LEO, MBUNGE AWEKWA RUMANDE




 mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwasili  eneo la vurugu kabla  ya kuanza kwa  vurugu  hizo
 Mbunge Msigwa akiondoka  eneo la mashine  tatu 

 Machinga  wakisukuma gari ya  mbunge Msigwa 

 Polisi  wakimfuatilia  mbunge Msigwa kwa  nyuma baada ya  kufika eneo hilo  bila kufanya biashara kama alivyoahidi

Polisi  wakianza  kufukuza  wananchi  eneo hilo


 Polisi  wakipita  eneo la Mashine  tatu asubuhi 
 Abiria  na  wapiga  debe  stendi kuu  wakinawa maji baada ya  kupigwa mabomu na kumwagiwa maji ya kuwasha  na askari  wa FFU leo




 Hali  ikiendelea  kuwa  tete  kwa machinga  kufunga barabara  kuu  ya  Iringa  Dodoma na ile ya mashine  tatu
Ni Machafuko  Iringa  hivi  leo








View detail

Wednesday, May 15, 2013

Serikali ya Mali yachangishiwa pesa na EU kusaidiwa

Mali yaomba msaada kufadhili harakati za kijeshi

Zaidi ya wajumbe 100 wanakutana mjini Brussels, Ubeljiji kuchangisha fedha kutolewa kama msaada utakaotolewa kwa nchi ya Mali. Hili ndilo kongamano la kwanza tangu wanajeshi wa Ufaransa kuanzisha opesheni kazkazini mwa Mali dhidi ya wapiganaji wa kiiisilamu waliotwaa nusu ya maeneo ya nchi.

Wanajeshi wa Ufaransa waliingia ndani ya Mali kukabiliana na wapiganaji wa kiisilamu wenye uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda.
Wapiganaji hao walifanikiwa kuthibiti maeneo ya kaskazini mwa Mali kutokana na udhaifu wa serikali iliyolaumiwa kuwa kujihusisha zaidi na ufisadi. Kipao Mbele kwa sasa ni jinsi ya kufanya mageuzi kwenye jeshi na tasisi nyingine za taifa.
Kumekua na shinikiza kwa Mali kuandaa uchaguzi mkuu wa kidemokrasia ifikapo mwezi Julai, japo raia wengi wameelezea ugumu wa kuafikiwa hilo.
Shirika la misaada la Oxfam limesema kwamba Mali itahitaji msaada kwa miaka 15 ijayo, ili kuafikia malengo yanayotarajiwa.

Licha ya juhudi za sasa, kungali na msukosuko wa kisiasa Mali, Kaskazini mwa Mali waafrika Weusi wamelalamikia kugabuliwa na jamii za kiarabu na Tuareg.
Kwa upande mwingine Tuareg na Waarabu wamelalamikia kubaguliwa na serikali Kuu iliyoko Bamako. Wafadhili wanasema ni muhimu kuwepo, na maridhiano kati ya jamii zote.mak
View detail

Tuesday, May 14, 2013

Waandamanaji Kenya Wawalinganishwa Wabunge wa Kenya na 'Nguruwe'

Wananchi wa Kenya wanaopinga wabunge kuongezwa mishahara

Polisi nchini Kenya wamekabiliana na waandamanaji waliozingira majengo ya bunge kulaani jaribio la wabunge kutaka kujiongeza mishahara.
Polisi hao wametumia gesi ya kutoa machozi pamoja na maji kuwatawanya waandamanaji hao ambao wengi wao ni wanachama wa mashirika ya kijamii ambao wamesma katu hawaondoki katika majengo hayo ya bunge hadi wabunge watakapopata ujumbe wao.

Pia inaarifiwa kuwa wanawataka wabunge kutia saini na kuapa kuwa hawatatumia bunge kunyanyasa wananchi maskini kwa kujiongeza mishahara kinyume na sheria.
Mashirika ya kijamii yaliandaa maandamano hayo kuonyesha ghadhabu waliyonayo wakenya dhidi ya wabunge hao wanaotaka kuongezwa miashara, miezi miwili tu baada ya kufanyiika uchaguzi mkuu wa amani.
Aidha waandamanaji hao walipeleka Nguruwe kwenye mlango mkuu wa kuingia katika bunge pamoja na damu kama ishara kuwa wabunge ni watu walafi na wasiojali maslahi ya wakenya kwa kujitakia makubwa.
Maandamano haya yanakuja siku moja baada ya tume ya kitaifa ya mishahara ambayo wajibu wake ni kudhibiti mishahara ya wafanyakazi wa umma kusema kuwa katu haitawaongeza mishahara wabunge.
Tume hiyo ilisema siku ya Jumatatu kuwa haitaogopa vitisho vya wabunge kutaka kuivunjilia mbali tume hiyo ikiwa hawatawaongeza mishahara wabunge kama kikwazo.
Wabunge hao walijaribu kwa kutumia vitisho kuilazimisha tume hiyo kuwoangeza mishahara lakini hawakufua dafu.

Ni baada ya mbunge mmoja kuwasilisha hoja bungeni kuwa ikiwa tume hiyo haitawaongeza mishahara watafanyya kila hali kuivunja.
Hata hivyo tume hiyo ni ya kikatiba.
Wabunge wa Kenya wanataka kulipwa mshahara wa shilingi 850,000 wakati wakihudumu katika bunge la kumi ikipuuza mshahara waliowekewa na tume ya mishahara ambao ni shilingi 532,000. Wanasema pesa hizi ni kidogo sana.
View detail

RAIA WA USWISWI NA WANAWAKE 11 WA KENYA WAANDAA FILAMU YA MAPENZI NA MBWA

Wafanyakazi wa migodini wafanya Mgomo Afrika Kusini

Kuna hofu kuwa huenda maandamano kama yaliyoshuhudiwa mwaka jana yakatokea

Kampuni ya uchimbaji madini ya Lonmin, nchini Afrika Kusini inasema kuwa maelfu ya wafanyakazi katika mgodi wake wa wa platinum wamefanya mgomo kinyume cha sheria baada ya afisa wa muungano wao kupigwa risasi katika baa moja mwishioni mwa juma.
Msemaji wa kampuni hiyo Sue Vey amesema kuwa shughuli zote za uzalishaji kwenye kiwanda hicho zimevurugika .
Mgomo huu umezua hofu ya vurugu zaidi kutokea baada ya sekta hiyo kukumbwa na migomo mwaka jana
Mwezi Agosti mwaka jana wafanyakazi thelathini na wanne waliuliwa na polisi katika mgodi wa Marikana na waandishi wa habari wanasema mgomo huo umesababisha hofu ya kutokea kwa ghasia kufuatia hali ya taharuki iliyopo juu ya kukatwa kwa kazi , mashauriano ya riba na uhasama ndani ya muungano wa wafanyakazi.
Lonmin, ambayo hisa zake,ziko katika soko la hisa la London na Johannesburg , ndiyo kampuni ya tatu kwa ukubwa katika kuzalisha madini ya platinum.
Taarifa za mgomo wa leo zimesababisha hisa za kampuni hiyo kushuka kwa asilimia 5% mjini London.
Msemaji wa kampuni hiyo, Sue Vey alisema kuwa migodi yote kumi na mitatu ya kampuni hiyo imefungwa kwa sasa.

"Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliwasili kazini ingawa hawakuelekea katika shughuli zao kama ilivyo desturi yao
Huku akisema kuwa kampuni hiyo haielewi kwa nini wafanyakazi wameamua kugoma, msemaji wa chama cha wafanyakazi hao, alisema kuwa huenda mgomo huo unatokana na ghadhabu ya wafanyakazi hao, kuhusu mauaji yaliyotokea mwishoni mwa wiki ya kiongozi mmoja wa chama hasimu cha wafanyakazi.
Polisi walithibitisha kuwa kiongozi huyo aliuawa mwishini mwa wiki katika eneo Rustenburg.
View detail

KITUO CHA TAASISI YA KIMATAIFA YA KILIMO CHA KITROPIKI (IITA) DAR ES SALAAM CHAZINDULIWA NA MH RAIS KIKWETE

Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chifu Olesegun Obasanjo akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam jana Mei 13, 2013.
 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa wakionja mikate iliyotengenezwa kwa unga wa muhogo wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam jana Mei 13, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mazungumzo na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo baada ya uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam jana Mei 13, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa
wakisikiliza maelezo ya kitaalamu juu ya utafiti wa maradhi ya migomba toka kwa Profesa Rony Swennen wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam jana Mei 13, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam jana Mei 13, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam jana Mei 13, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo wakiangalia mashine ya kuvunia mihogo
 
Wadau wakionja vyakula mbalimbali vinavyotengenezwa kwa unga wa muhogo
 
Wadau wakiwa katika sherehe hizo
Mmoja wa watafiti akielezea kazi yake kituoni hapo
 
Watafiti wakielezea kazi zao
 
Wadau wa ITTA ambao ni wapenzi wa Globu ya Jamii
 
Wadau shereheni
 
Wageni waalikwa
 
 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo wakifungua kituo hicho
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete achunguza kitu kwa kutumia kifaa cha kisayansi katika taasisi hiyo.
 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Benjamin Mkapa pamona na Balozi wa Marekani nchini Tanzania wakiagalia sehemu ya vifaa vya kisayansi katika taasisi hiyo.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo wakifungua kituo hicho
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo pamoja na Rais Mstaafu,Mh. Benjamin Mkapa wakizindua rasmi jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam jana Mei 13, 2013.
 
Picha ya pamoja.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo baada ya uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam jana Mei 13, 2013.
View detail

Thursday, May 9, 2013

SHEKH PONDA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Mahakama ya Kisutu leo hii imetoa hukumu ya Shekh Ponda kwa kumuhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja (1) na kuwaachia huru wenzake 49, kutokana na hukumu hiyo kauli yake ya Allah ndio hakimu mkuu kuliko wote ameidhihirisha pale alipowaona wafuasi wake wakimlaki kwa furaha huku wakiendelea kupiga TAQBIR na kusema hakika Allah ndiye pekee wa kumuomba na kila uongo na Unafiki utajitenga na ukweli utajidhihirisha!!! wakati ukifika hakuna wakupinga! alimalizia kwa kusema ALLAH AQBAR!! 

Ulinzi mkali uliimarishwa ili kudhibiti hatua yoyote isiyo ya kawaida ktk kumlaki shekh Ponda ambae amekadiriwa kua na wafuasi takribani 10,000 kwa mkoa wa Dar es salaam pekee na wengine wakiwa mikoani, kutokana na hilo ulinzi ktk eneo la mahakama uliimarishwa na kua tayari kwa lolote litakalojitokeza kutokana na furaha za wafuasi hao wa Shekh Ponda.
Baadhi ya Umati wa wafuasi wa Shekh Ponda  mjini Dar es salaam


View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop