Wafuasi wa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi |
Wafuasi wa rais wa Misri
aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi wamefanya maandamano makubwa
mjini Cairo, huku waumini wa dini ya Kiislamu wakiadhimsiha Ijumaa ya
kwanza tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Wafuasi wa kiongozi huyo wa vugu vugu la Muslim
Brotherhood walijikusanya Mashariki mwa mji huo, kushinikiza utawala wa
kijeshi kumrejesha madarakani kiongozi wao.Wapinzani wa rais huyo wa zamani ambao waliandamana hadi rais huyo akaondolewa madarakani na jeshi watakusanyika katika medani ya Tahrir.
Watu kadhaa wameuawa kwenye ghasia zilizotokea tangu Morsi alipoondolewa.
Mwandishi wa www.azizicompdoc.blogspot.com mjini Cairo, anasema vuguvugu la Muslim Brotherhood huenda liliwatenga raia wengi wakati wa utawala wa Morsi, lakini bado raia wengi wa nchi hiyo hawataki jeshi kuingilia masuala ya siasa.
Marekani kutuma ndege za kivita Misri
Siku ya Alhamisi serikali ya Marekani, ilitoa wito kwa utawala mpya wa Misri, kusitisha harakati zake za kuwakamata wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood na kuonya dhidi ya kulenga kundi lolote.Wanajeshi wakishika doria mjini Cairo |
Hata hivyo msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney amesema, utawala wa Washington hauamini kuwa ni lazima isitishe misaada yake ya Misri.
Marekani inatarajiwa kupeleka ndege nne za kivita aina ya F-16 nchini Misri, lakini haijathibitisha kuwa msaada huo utatolewa lini.
Serikali ya Marekani imesema, inachunguza ikiwa aumuzi huo wa jeshi la Misri kumuondoa madarakani rais Morsi ni mapinduzi ya Kijeshi kwa kuwa sheria za Marekani inazuia serikali kutoa misaada kwa nchi yoyote ambayo kiongozi aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia ataondolewa kupitia mapinduzi.
Wafuasi wa rais Morsi wamekuwa wakiandamana wiki nzima karibu na kambi ya kijeshi iliyoko Mashariki mwa mji mkuu wa Cairo, ambako wanaamini kuwa kiongozi wao anazuiliwa na maafisa wa kijeshi tangu alipoondolewa madarakani.
0 comments:
Post a Comment