Welcome to our online store Portal

Template Information

Tuesday, July 9, 2013

SOKO KUBWA LAWAKA MOTO MOGADISHU


Gari limelipuka ndani ya soko rasmi mjini Mogadishu nchini Somalia.
Kwa mujibu wa polisi, hakuna taarifa zaidi kuhusu waliojeruhiwa katika shambulizi hilo kwenye soko la Bakara.
Walioshuhudia shambulizi wanasema kuwa gari lilikuwa limewabeba watu waliokuwa wamevelia magwanda ya jeshi.
Hakuna kundi lolote limekiri kufanya shambulizi hilo, lakini kundi la wapiganaji wa kiisilamu wa al-Shabab, limekuwa likifanya mashambulizi ya kuvizia tangu kuondolewa kutoka mjini Mogadishu mwaka 2011.
Polisi walifahamisha azizicompdoc.blogspot.com kuwa afisaa mkuu wa polisi amejeruhiwa kwenye shambulizi hilo, lakini hakuna taarifa zaidi hadi uchunguzi utakapokamilika.
Afisaa wa polisi Mohamed Hussein, alisema bomu lilikuwa limefichwa ndani ya gari la kijeshi, na limewajeruhi wanajeshi watano wa serikali.
Naye Hussein Nur, ambaye ni mfanyabiashara wa pesa, alisema alishuhudia gari likilipuka.
Kundi la Al-Shabab linapigana likitaka kuruhusiwa utawala wa kiisilamu nchini Somalia na licha ya kufurushwa kutoka mji mkuu Mogadishu katika miaka miwili iliyopita,lingali linadhibiti sehemu kubwa ya nchi.
Wanajeshi 18,000 wa Afrika, wako nchini Somalia kuunga mkono serikali ya Somalia iliyo chini ya rais Hassan Sheikh Mohamud, aliyechaguliwa na wabunge mwaka jana.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop