Monday, September 16, 2013

Dr Jabir Kuwe Bakari ajitoa Bodi ya Bandari

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ameipangua Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuwaondoa wajumbe sita kati ya wanane kwa lengo la kuondoa migongano isiyo na tija ndani ya mamlaka hiyo.

Amewateua wajumbe wapya watatu na kusababisha iwe wajumbe watano ambao ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Mwakilishi wa wafanyakazi wa TPA ambao hakuwataja majina.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana, wajumbe waliondolewa ni Julius Mamiro, John Ulanga, Caroline Kavishe, Dk. Hildebrand Shayo na Asha Nasoro.
Dk. Mwakyembe pia amekubali ombi maalum la Dk. Jabiri Kuwe Bakari ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e-Government, la kujitoa kwenye ujumbe ili aelekeze nguvu zake katika kuiimarisha taasisi yake ambayo huduma zake zitanufaisha idara na taasisi zote za Serikali ikiwamo TPA.

Katika mabadiliko hayo, Dk. Mwakyembe  amewabakiza wajumbe wawili ambao ni Saidi Sauko na Jaffer Machano.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About