Wednesday, September 25, 2013

MWANAMKE ABAKWA MALI NA WANAJESHI WA UN

Kikosi cha wanajeshi cha Minusma nchini Mali kiko chini ya UN
Umoja wa Mataifa unasema kuwa wanajeshi wake wanne wa amani nchini Mali walihusika na kitendo cha kumbaka mwanamke mmoja wiki jana.
Wanajeshi hao ni sehemu ya wanajeshi 1500 wa Umoja wa Mataifa kutoka Chad ambao wanafanya kazi chini ya kikosi cha Minusma. Umoja wa Mataifa unataka serikali ya Chad kuchunguza madai hayo ili kuwachukulia hatua za kinidhamu watakaopatikana na hatia.
Inasemekana mwanamke aliyebakwa alikuwa amekuja kutafuta msaada wa kimatibabu kutoka kwa Umoja wa Mataifa punde baada ya kubakwa Alhamisi wiki jana mjini Gao.
Madai ya mwanamke huyo yalisababisha hatua za haraka za kuchunguza washukiwa.
Haijulikani idadi ya wanajeshi wa Chad waliohusika na shambulizi hilo, lakini mwathiriwa aliweza kuwatambua wanajeshi wanne kuwa miongoni mwa wale waliombaka katika chumba kilichokuwa karibu na baa.
Wakati wa tukio hilo, wanajeshi miamoja na sitini na tano, walikuwa wakishika doria mjini Gao.
Walikiuka amri ya wakuu wao ya kutoondoka kambini katika eneo la Tessalit, Kaskazini mwa nchi, kufuatia tofauti zilizoibuka kuhusu mazingira katika kambi hiyo.
Msemaji wa Minusma mjini Bamako alisema kuwa ilikuwa juu ya jeshi la Chad kuamua adhabu watakayopewa wanajeshi hao,
Alisema kuwa mwathiriwa atapokea matibabu na ushauri nasaha pamoja na msaada wa kisheria lakini sio msaada wa kifedha.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About