Wakati viongozi wa Kenya na Sudan wakikabiliwa na kesi huko ICC, viongozi wa nchi za Afrika wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuwa mahakama hiyo inafanya upendeleo na kuwaonea kwa makusudi.
AU ilijadili uwezekano wa nchi wanachama kujitoa, lakini wazo hilo halikuungwa mkono kiasi cha kutosha.
Wanasiasa na wanadiplomasia waandamizi akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan wamekosoa mpango wa kujitoa kutoka ICC.
Viongozi hao wa AU, waliokutana Addis Ababa, walikubaliana kuwawekea kinga ya kutoshitakiwa kiongozi yoyote wa taifa la Afrika.
Pia wameitaka Kenya iandike barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiga kuomba ucheleweshwaji wa kesi katika mahakama ya ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya jinai.
0 comments:
Post a Comment