Tuesday, October 15, 2013

WAKRISTO MALAYSIA WATAKA KUTUMIA JINA ALLAH LINALOTUMIKA NA WAISLAM

Waumini wa dini ya kiisilamu wakipinga matumizi ya jina Allah kwa kikristo
Mahakama nchini Malaysia, imeamua kuwa watu wasio waisilamu wasitumie jina 'Allah' kumaanisha Mungu katika katika imani zao na kubatilisha uamuzi wa mahakama ndogo uliotolewa mwaka 2009.
Mahakama ya rufaa ilisema kuwa jina Allah linapaswa tu kutumiwa na waumini wa kiisilamu la sivyo linaweza kuzua taharuki miongoni mwa jamii.
Watu wa imani zote nchini Malaysia wanatumia neno Allah kumaanisha Mungu.
Wakristo wanateta kuwa wamekuwa wakitumia jina hilo la Allah katika lugha ya Malay na ambalo lilitokana na lugha ya kiarabu kumaanisha Mungu kwa miaka mingi na kuwa uamuzi wa mahakama unakiuka haki zao.
Mwanamke mmoja mkristo alisema kuwa uamuzi huo utaathiri jamii pakubwa.
"ikiwa tutawazuia watu wengine kutumia jila la Allah, basi itatubidi kutafsiri Bibilia nzima upya" Ester Moiji kutoka jimbo la Sabah aliambia www.azizicompdoc.blogspot.com
Umauzi ulitolewa na mahakama ndogo mwaka 2009 ulisababisha taharuki baina ya waisilamu na wakristo huku makanisa na misikiti ikishambuliwa.
Ilitokea baada ya serikali kusema kuwa jarida la kikatoliki la The Herald, haliwezi kutumia jina Allah katika makala yake ya lugha ya Malay kumaanisha Mungu kwa kikristo.
Wahariri wa jarida hilo lilikwenda mahakani kupinga uamuzi huo na mahakama ikafanya uamuzi uliowapendelea. Serikali baadaye ilikata rufaa.
Lakini katika uamuzi wake leo, jaji alisema kuwa jina Allah haliwezi kutumika kwa dini ya kikrsito kumaanisha Mungu na kuwa ikiwa jina hilo litatumiwa basi huenda likazusha taharuki baina ya jamii.
Mhariri wa jarida hilo alisema kuwa alighadhabishwa na kushangazwa sana na uamuzi wa mahakama na kwamba atakata rufaa.
Wafuasi wa jarida hilo wamesema kuwa Bibilia zilizoandikwa kwa lugha ya Malay zimekuwa zikimtaja Allah kumaanisha Mungu kwa kikristo tangu zamani sana.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About