Welcome to our online store Portal

Template Information

Friday, October 11, 2013

RAIS BANDA AVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI KWA UFISADI

Rais wa Malawi, Joyce Banda amelifuta kazi baraza lake la mawaziri kutokana na kuongezeka kwa visa vya ufisadi serikalini.
Maafisa wa serikali wamekuwa wakipatikana na pesa zikiwa zimefichwa chini ya vitanda vyao na kwenye magari yao, kwa mujibu wa mwandishi wa www.azizicompdoc.blogspot.com.
Mwezi jana afisaa mmoja mkuu katika wizara ya fedha Paul Mphwiyo, aliyeonekana kuwa afisaa mmoja mkuu serikali ambaye anaonekana kupinga sana ufisadi, alipigwa risasi na kujeruhiwa.
Wahisani wa kimataifa wamekuwa wakimtaka rais Banda kuchukua hatua kukabiliana na ufisadi.
Malawi ni taifa masikini na hutegemea sana msaada kutoka kwa Muungano wa Ulaya na nchi zengine za kimagharibi.
Bi banda amesema kuwa mawaziri wapya watateuliwa hivi karibuni bila ya kutoa maelezo zaidi.
Aliitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri kabla kutangaza kulivunja.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari Banda alisema kuwa ameunda jopo maalum likijumuisha polisi na maafisa wa serikali kufanya ukaguzi wa matumizi ya pesa za serikali katika idara zote za serikali.
Mwandishi wa www.azizicompdoc.blogspot.com. nchini humo anasema kupigwa risasi kwa bwana Mphwiyo ndio ilikuwa mwanzo wa taarfa kuwa baadhi ya maafisa wa serikali wanashirikiana na wafanyabisahara kuifilisi serikali katika utoaji wa kandarasi na mikataba bandia.
Washukiwa wanne walikamatwa kuhusiana na kupigwa risasi kwa afisa huyo.
Takriban maafisa kumi wa serikali wama
ekamatwa wakisubiri kusikilizwa kwa kesi zao kuhusiana na ufisadi.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop