Welcome to our online store Portal

Template Information

Wednesday, October 9, 2013

LIBYA YAOMBA MSAADA HALI NI TETE


Ali Zeidan Waziri mkuu wa Libya  amezitaka nchi za Magharibi kuisaidia kukomessha kuenea kwa makundi ya wapiganaji wenye ikitadi kali nchini humo.
Kwenye mahojiano na azizicompdoc.blogspot.com Bwana Zeidani alisema kuwa Libya inatumika kama sehemu ya kusambazia silaha katika kanda nzima.
“Hizi silaha zinapelekwa kwa wingi katika nchi jirani kwa hivyo lazima pawepo ushirikiano wa kimataifa kukomesha jambo hilo,’’ alisema bwana Zeidan.
Mnamo siku ya Jumatatu serikali ya Libya ilimhoji balozi wa Marekani nchini humo kuhusu kukamatwa kwa mshukiwa wa ugaidi na mmoja wa viongozi wa kundi la al-Qaeda mjini Tripoli.
Anas al-Liby, alikuwa anasakwa kwa kuongoza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 na baada ya zaidi ya miaka kumi aliweza kukamatwa mjini Tripoli na makomando wa Marekani.
Marekani imetetea hatua ya kukamatwa kwa gaidi huyo ikisema kuwa kilikuwa kitendo halali kuambatana na sharia za kimataifa.
Lakini bunge la Libya Jumanne lilitaka al Liby kurejeshwa nchini humo likitaja kukamatwa kwake kama kitendo cha utekaji nyara na kupuuza utawala wa Libya.
Rais Barack Obama aliambia waandishi wa habari Jumanne kuwa Marekani ina ushahidi wa kutosha kuonyesha kua Al Liby alipanga na kusaidia katika kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani na kuwaua watu wengi sana.
Obama aliongeza kuwa Al Liby atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop