Welcome to our online store Portal

Template Information

Thursday, October 3, 2013

NCHI ZA AFRIKA ZITAUNGANA NA KENYA KUJITOA ICC?



Kikao cha dharura kujadili hoja ya Kenya kitafanyika mjini Addis Ababa katika makao makuu ya AU
Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kukutana mwezi ujao mjini Addis Ababa Ethiopia, kujadili msimamo wa bara hili kuhusu iwapo watajiunga na Kenya katika kujiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifiu - ICC.
Mkutano huo unafuatia ombi la Kenya kutaka kikao cha dharura cha Umoja wa Afrika kujadili kesi zinazowakabili Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.
Mwandishi wa www.azizicompdoc.blogspot.com mjini Addis Aabab, anasema kuna dalili kuwa ombi hilo la Kenya limeanza kuungwa mkono na mataifa mengi barani.
Kwa sasa hakuna dalili kuwa kuna msimamo mmoja kuhusu ikiwa wanachama 54 wa Muungano wa Afrika waliotia saini mkataba wa Roma wanataka kujiondoa, lakini marais wa nchi hizo bado watajadili uwezekano wa wanachama 34 wa mkataba wa Roma uliounda mahakama ya ICC watajiondoa ICC.
Tangu kuanza kwa kesi ya Naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya ICC wiki jana, na ile ya Rais Kenyatta ikitarajiwa kuanza mwezi Novemba, dalili zimeonekana kuwa wengi hawana imani na mahakama hiyo wakiiona kama chombo cha nchi za Magharibi kukandamiza waafrika.
Kikao cha dharura sasa kimepangwa kujadili swala hilo baada ya Kenya kuonekana kutaka kuungwa mkono katika azma yake ya kujiondoa ICC.
Kuna uwezekano wa nchi wanacahama wa mkataba wa Roma kujiondoa ICC lakini bado kuna nafasi ya maombi mengine kufanywa kuhusiana na hilo.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop