Thursday, October 3, 2013

ULAYA YAGEUKA MAKABURI YA WAAFRIKA


Takriban wahamiaji 130 wa kiafrika mefariki na wengine wengi hawajulikani waliko baada ya boti iliyokuwa inawabeba kuelekea Ulaya kuzama katika pwani ya Utaliana
Wahamiaji wakiokolewa kutoka baharini

Maafisa katika kisiwa kikubwa cha Sicily katika bahari ya Meditarenia wanasema kuwa wamepata maiti 130 baada ya mashua iliyokuwa imewabeba takriban wahamiaji 500 wa kiafrika kushika moto na kuzama katika kisiwa cha Lampedusa.
Boti hiyo ilikuwa safarini kuelekea Ulaya lakini ikazama katika kisiwa cha Lampedusa katika pwani ya Utaliana
Takriban miili 103 imepatikana baharini na mingine zaidi kupatikana ndani ya boti iliyozama.
Inaarifiwa abiria walijirusha baharini wakati moto ulipozuka ndani ya boti
Zaidi ya wahamiaji 150 wameokolewa.
Wengi wa wahamiaji hao walikuwa raia wa Eritrea na Somalia,kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Shughuli kubwa ya uokozi ingali inaendelea kuwatafuta manusura kwani inahofiwa mamia zaidi huenda wamefariki kutokana na ajali hiyo.
Meya wa mji huo anasema kuwa walionusurika wako hatika hali ya mshutuko na walimwambia kuwa moto mdogo uliwashwa baada ya meli kukwama na lengo lilikuwa kuitisha msaada.
Lakini alisema kuwa moto ulisambaa kupita kiasi na ikawa vigumu kuudhibiti.
Kisiwa cha Lampedusa kiko kati ya Tunisia na Sicily na kimekuwa kiingilio kikuu cha wahamiaji kuingia barani Ulaya.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About