Friday, October 25, 2013

Wananchi Madagascar wajitokeza kumchagua Rais


Harakati za kampeni kabla ya uchaguzi wa Rais Madagascar
Wananchi wa Madagascar wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa kwanza kufanyika nchini humo tangu yalipofanyika mapinduzi yaliyoungwa mkono na jeshi miaka minne iliyopita.
Wagombea 33 wanawania urais wa nchi hiyo katika uchaguzi huo, ambao umeahirishwa mara tatu mwaka huu.
Wagombea wawili wanaopewa nafasi ya kushinda, wanaahidi kujenga upya uchumi wa Madagascar baada ya miaka ya mgogoro wa kisiasa na kiuchumi.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, zaidi ya asilimia 92% ya wananchi milioni 21 wa Madagascar wanaishi chini ya dola mbili kwa siku.
Rais Andry Rajoelina alimng'oa madarakani Marc Ravalomanana mwaka 2009, na kulitumbukiza taifa hilo katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kusababisha nchi hiyo kutengwa na jumuiya ya kimataifa na kunyimwa misaada kutoka nje.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About