Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa GEPF Bw.Daudi Msangi akifafanua
kuhusu fursa inayotolewa na Mfuko huo kwa raia wa Kigeni wanaoishi na
kufanya kazi Nchini ambapo wanaweza kujiwekea akiba katika mfuko
huo,kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi. Fatma Salum.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa GEPF bw.Daudi Msangi akiwaeleza
waandishi wa habari Jijijini Dar es Salaam kuhusu mfumo mpya
unaowawezesha wananchi wasio katika sekta rasmi kujiunga na mfuko huo na
kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo,kushoto ni
Meneja Masoko na Huduma wa Mfuko huo bw.Aloyce Ntukamazina.(Picha na
Frank Mvungi)
Na Fatma Salum-Maelezo.
Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii GEPF umetoa fursa kwa wananchi walio katika Sekta
isiyo rasmi kujiunga na mfuko huo ili kunufaika na mafao mbalimbali
yanayotolewa.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo
Bw.Daudi Msangi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
maboresho yanayofanywa na mfuko huo ili kuwanufaisha wanachama wake.
Bw.
Msangi alibainisha kuwa wanachama wanaojiunga na mfuko huo toka sekta
isiyo rasmi wanao uhuru wa kuamua ni kiasi gani watachangia katika
mfuko kulingana na vipato vyao ili kujiwekea akiba .
Aidha alisema mfuko huo utaanza kutoa pensheni kwa wanachama wa hiari watakaochangia kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.
Akifafanua
zaidi Bw Msangi alisema mfuko huo umepanua wigo kwa kuwapa nafasi raia
wa kigeni kujiunga na mfuko ili wajiwekee akiba katika kipindi
watakachokuwa wakifanya kazi hapa nchini.
Aliongeza
kuwa Mfuko huo pia umetoa fursa kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi
kujiunga na mfuko na kujiwekea akiba kwa faida ya maisha yao ya baadae
hasa wanapostaafu na pia kuwapa uwezo wa kuendesha maisha yao
watakaporudi nchini.
Bw.Msangi
alitaja baadhi ya mafao yanayotolewa na mfuko huo kuwa ni mafao ya
warithi,mafao ya kuumia kazini, fao la elimu na msaada wa mazishi na
kuongeza kuwa kwa sasa thamani ya mfuko huo ni shilingi bilioni 210 na
inatarajiwa ifikapo mwakani thamani itaongezeka hadi shilingi bilioni
250.
0 comments:
Post a Comment