Tuesday, November 26, 2013

JOPO LA USULUHISHI WA MIGOGORO LAKUTANA NA RAIS KIKWETE


c4
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea mbele jopo la Marais wastaafu wa Afrika kuhusu  linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe Joaquim Chissano anayefuatana na Rais Mstaafu wa Botswana Mhe Festus Mogae leo Novemba 25, 2013 Ikulu jijjini Dar es salaam. Mhe. Chissano, ambaye ni mwenyekiti wa Jopo hilo pamoja na Mhe Mogae, walifika Ikulu kusikiliza upande wa Tanzania kuhusu mgogoro wa mpaka na nchi ya Malawi, baada ya kufanya hivyo hivi karibuni huko Blantyre.(PICHA NA IKULU).
c5
c6

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi amefanya mazungumzo na Bibi Mary Robinson, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) katika eneo la Maziwa Makuu.
Mazungumzo baina ya Rais Kikwete na Bibi Robinson yamehusu maendeleo na hatua iliyofikiwa katika mgogoro wa Mashariki mwa DRC – Congo na jitihada zinazofanywa za kutekeleza mkataba wa amani ambapo Tanzania imetoa mchango mkubwa katika jitihada hizo. 

“Nakupongeza kwa juhudi zako katika masuala ya amani katika nchi za Maziwa Makuu na pia nakuomba uendelee kutoa mchango wako zaidi wa mambo gani muhimu ya kuzingatia baadae. Bibi Robinson pia amempa salamu za rambirambi Rais Kikwete pamoja na familia za wanajeshi waliopoteza maisha yao katika harakati za kuleta amani huko mashariki mwa DRC Congo.
Bibi Robinson amemuomba Rais Kikwete aendelee kutoa mchango wake kwenye juhudi za kuleta amani nchini Congo baada ya kikosi cha UN kufanikiwa kuwaondoa waasi wa kikundi cha M23 kutoka Mashariki mwa  DRC – Congo.

Viongozi hawa wamekubaliana kuwa ipo haja ya kuendeleza juhudi za kuleta amani  DRC na kuangalia jinsi ya kusonga mbele na kubainisha mahitaji na hatua zaidi za kuchukua katika kuhakikisha amani  na usalama vinapatikana na hatimaye kujenga uchumi wa DRC.
Wakati huo huo Rais Kikwete amekutana na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mheshimiwa Joachim Chissano  ambaye ni msuluhishi wa mgogoro wa Mpaka Kati ya Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa.  Rais Chissano na ujumbe wake upo nchini kusikiliza hoja za Tanzania kuhusu mpaka wa Ziwa Nyasa ambapo Rais Kikwete amewasilisha hoja zake kwao. Tayari msuluhishi huyo ameshasikiliza hoja za Malawi ambapo inatarajiwa hoja za nchi zote mbili hizi zitatafsiriwa na kuzingatiwa katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo wa Ziwa Nyasa.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About