Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa Mbinga Magharibi
Kapteni John Komba kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Mbeya kwa
meli ya MV Songea.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipuliza vuvuzela pamoja na wananchi wa Mbamba B waliokuja
kuusindikiza msafara wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana,ambao
umemaliza ziara ya mkoa wa Ruvuma na kuanza safari ya kuelekea mkoa wa
Mbeya .
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha -Migiro akitoa salaam za
shukran kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa ukarimu wao wa muda wote wa
ziara na kuwatakia maisha mema.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya
Nyasa mkoani Ruvuma kabla ya kupanda meli kuelekea wilaya ya Kyela
mkoani Mbeya.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa wilaya ya
Nyasa na kuwaambia serikali imeshaagiza meli ya tani 400 ambayo ipo
kwenye matengenezo sasa na ikikamilika italetwa ziwani hapo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na ujumbe wake pamoja na
viongozi wa CCM mkoa wa Ruvuma kabla ya kupanda meli kuelekea Kyela
mkoani Mbeya.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye wakiaga wananchi wa wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma tayari kwa
safari ya kuelekea Kyela mkoani Mbeya.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Katibu wa Nec
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwaaga wananchi wa wilaya ya Nyasa
wakati wakiondoka kwenye bandari ya Mbamba bay kuelekea Nyasa.
”Kwa Herini wana Nyasa”msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ukiwaaga wananchi wa wilaya ya Nyasa.
Ni
siku ya Kihistoria kwa CCM na Wana Nyasa kwani matumaini yameongezeka
kwa wananchi hao baada ya viongozi wao wa Kitaifa kuwa nao kwa muda wa
siku tisa mkoani Ruvuma.
0 comments:
Post a Comment