Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akiongozana na Balozi
Katiti wa shina namba moja la Kata ya Sange wilayani Ileje Mkoani Mbeya
ambapo katibu mkuu huyo alizungumza na wanachama wa shina hilo na
kumpongeza balozi kwa kazi nzuri ya kujitolea na kukijenga chama cha
Mapinduzi, amewataka viongozi wote wa mikoa, wilaya na kata kuwatembelea
mabalozi .Ili kuwapa moyo na kutambua umuhimu wa kazi zoa kwani hao
ndiyo wenye wanachama lakini viongozi wa juu hawana wanachama kazi yao
ni kuongoza na kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi
inatekelezwa kwa mafanikio ili kuwapa maendeleo wananchi, Katika ziara
hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameongozana na Katibu
wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa..
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kushoto akipata maelezo ya
Mkuu wa wilaya ya Ileje Rosemary Sinyamule wakati alipokagua daraja la
mto Songwe katika mpaka wa Tanzania na Malawi mahali ambapo kunatakiwa
kujengwa ofisi ya uhamiaji ili kurahisisha kazi za tasisi hiyo muhimu
nchini, Wilaya ya Ilenje kata ya Isongole inapakana na kata na kijiji
cha Mbilima wilaya ya Chitipa kwa upande wa Malawi
Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kalembo
kutokana na kushindwa kutembelea na kuweka shada la maua katika kaburi
la marehemu Steven Kibona ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na
kutumikia nchi kwa uadilifu mkubwa, Kinana amesema yeye na marehemu
Steven Kibona waliwahi kufanya kazi wakiwa manaibu waziri wa Ulinzi na
akasifu uadilifu wa marehemu Steven Kibona kushoto ni Mke wa marehemu
Mama Kibona
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya
Kalembo
Mwenyekiti
wa halmashauri ya Kyela Bw. Mohamed Mwala wakati alipokuwa akitoa kero
ya mbolea inayotengenezwa na kiwanda cha Minjingu ambayo inadaiwa na
wakulima wa Ileje kuwa haina viwango na inasababisha mazao kuharibika.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mke wa Marehemu
Steven Kibona Mama Kibona kwenda kupata chakula cha mchana katika kata
ya Kalembo leo mchana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakivuka daraja
wakivuka daraja la mto Songwe wakati alipokagua daraja hilo hapo
wanaingia upande wa
Malawi.
Kikundi
cha ngoma ya asili ya watu wa Ileje kikitumbuiza kabla ya Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuzungumza na wananchi katika kata ya
Kalembo leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkuu
wa wilaya ya Ileje Rosemary Sinyamule wakati akitoa maelezo zaidi
kuhusu uimarishaji wa miundimbinu ya Wilaya ya Ileje ili kurahisisha
shughuliza kibiashara katika mpaka wa Tanzania na Malawi wakati
alipokagua daraja la mto Songwe katika mpaka huo leo kulia ni Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifana kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh. Godfrey Zambi.
Kutoka
kulia ni wapiganaji Richard Mwaikenda wa Jambo Leo, John Bukuku
Mkurugenzi wa Mtandao wa www.fullshangweblog.com na Laude Mwambona
kutoka gazeti la Mwananchi wakivinjari katika mpaka wa Malawi na
Tanzania wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua
daraja hilo wapiganaji hao ni miongozi mwa wanahabari waliopo katika
msafara huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakirejea upande wa Tanzania.
Maofisa wa Idara ya Uhamiaji wakiwa katika ofisi yao iliyopo Isongole inadaiwa jengo hilo ni la kupanga
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mkuu wa kituo hicho
cha idara ya uhamiaji Isongole Bw. Fredrick Luhanga wakati
alipotembelea katika ofisi hiyo.
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwa amekaa na wanachama wa CCM katika shina namba moja Kata ya Sange.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea nyumbani kwa balozi
Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kmataifana akishiriki ujenzi wa msingi wa jengo la kituo cha afya cha Lubanda
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa msingi wa jengo la kituo cha afya cha Lubanda leo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Bi Sylivia Siriwa
0 comments:
Post a Comment