Waasi wa M23 katika Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo wametangaza kumaliza uasi wao ndani ya nchi hiyo
muda mfupi baada ya kupigwa katika ngome yao ya mwisho na majeshi ya
serikali ya Congo yakishirikiana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa
kilichopewa uwezo wa kupigana na waasi hao.
Katika taarifa walioitoa waasi hao wamesema badala ya kufanya uasi sasa wataendesha harakati zao kutumia njia ya kisiasa.Muda mfupi uliopita Kiongozi wa waasi hao Bertrand Bisimwa ametangaza kuwaamuru mkuu wa wapiganaji wa M23 na makamanda wa vikosi vyote muhimu wa kundi hilo kuwaandaa wapiganaji wao kusalimisha silaha, kutawanyika kuondoka katika eneo la mapigano na kukubaliana na matakwa yatakayowekwa na serikali ya Congo
Awali Msemaji wa Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Lambert Mende aliambia www.azizicompdoc.blogspot.com kuwa majeshi ya nchi yameishambulia ngome ya mwisho ya waasi na wamekimbia na wengine huenda wakawa wamejisalimisha.
Majeshi ya serikali ya Kongo yakishirikana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupambana na waasi hao walianza mapambano dhidi ya M23 Octoba mwaka huu na kufanikiwa kuwaondoa katika eneo la Bunagana kwenye mpaka wa Uganda ambayo ni ngome yao muhimu.
0 comments:
Post a Comment