Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuili (aliyeshika mkasi) akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa vifaa vipya vya karakana za TEMESA mikoani.
Kushoto kwa Waziri ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA Eng.
Brig. Gen. Reginald Chonjo na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Marcelin
Magessa. Kulia kwa Waziri Magufuli ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi
Mhe. Eng. Gerson Lwenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Eng.
Mussa Iyombe, Mkurugenzi wa Vivuko wa TEMESA Eng. Japhet Masele na
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Umeme kutoka Wizara ya Ujenzi Eng.
Dkt. William Nsahama.
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuili (mbele) akionyeshwa na
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Marcelin Magessa (aliyeshika kipaza sauti)
baadhi ya vifaa vipya vilivyonunuliwa kwa ajili ya karakana za TEMESA
mikoani.
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuili (mbele) akionyeshwa na
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Marcelin Magessa (aliyeshika kipaza sauti)
baadhi ya vifaa vipya vilivyonunuliwa kwa ajili ya karakana za TEMESA
mikoani.
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuili akisalimiana na baadhi ya
Mameneja wa TEMESA mara baada ya kuongea nao wakati wa hafla ya
kukabidhi vifaa vipya vilivyonunuliwa kwa ajili ya karakana za TEMESA
mikoani.
Sehemu
ya Mameneja wa TEMESA kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini wakati wa
hafla ya kukabidhiwa vifaa vipya kwa ajili ya karakana za TEMESA
mikoani.
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pembe Magufuli amewataka Mameneja wa Wakala wa
Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) walioko mikoani na katika karakana
kuu za hapa Dar es Salaam za MT Depot na Vingunguti, kwamba ni budi wawe
wabunifu na wajitume wakati wakitekeleza majukumu waliyokabidhiwa
vinginevyo wizara yake haitasita kuwaondoa mara moja kuanzia sasa.
Waziri
Magufuli aliyasema hayo wakati akikabidhi vifaa vipya kwa ajili ya
karakana za TEMESA zilizoko mikoani. Vifaa hivyo vyenye thamani ya
Shilingi milioni 823.5 vimetolewa katika awamu mbili ambapo awamu ya
kwanza ilijumuisha mikoa ya Geita, Katavi, Iringa, Kilimanjaro, Tanga,
Shinyanga, Kigoma, Rukwa na Pwani.
Awamu
hii ya pili imejumuisha vifaa kwa ajili ya kazi za gereji za magari na
mitambo, shughuli za ufundi wa umeme, elektroniki na viyoyozi. Vifaa
hivyo vilivyokabidhiwa ni kwa ajili ya mikoa ya Tabora, Simuyu, Dodoma,
Mbeya, Arusha, Morogoro, Mara, Mtwara na vituo vya MT Depot na
Vingunguti vya hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Mameneja hao katika ofisi za TEMESA zilizoko Chang’ombe jijini Dar
es Salaam, Mhe. Magufuli alihoji kwamba “inashangaza kuona magari
yanatoka hapa Dar es Salaam na kupelekwa katika karakana ya TEMESA ya
Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya matengenezo, kwani hapa Dar es Salaam
kumetokea nini au mmebaki kuwa mawakala wa gereji binafsi tu?”.
Akifafanua
zaidi Waziri huyo alibainisha kuwa zipo baadhi ya gereji ambazo hazina
hadhi kabisa ya kutoa huduma hiyo lakini utakuta magari ya Serikali yako
huko na hata malipo yake hufanyika haraka haraka wakati yale ya TEMESA
hayalipwi na hakuna ufuatiliaji.
Aidha,
katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi alimpongeza Kaimu Meneja wa
Karakana ya TEMESA ya Bukoba mkoani Kagera kwa ubunifu na utendaji wake
mzuri kiasi cha kuvutia hata sekta binafsi kufanyia matenegezo magari
yao katika karakana hizo za Serikali. “Mtendaji kama huyu anatakiwa
kupewa kituo kamili” alielekeza Dkt. Magufuli na kumtaka Mtendaji Mkuu
wa TEMESA kutosita kumuondoa mtendaji yeyote anayeshindwa kutekeleza
majukumu yake inavyostahili.
“Ikibidi
tutakuwa tunawapangia vituo watendaji wazuri kama huyu wa Kagera hata
kama hawana digrii ili hawa wasomi waliopo ambao wameshindwakazi
wajifunze kutoka kwa hao wenye ubunifu” alimalizia Waziri Magufuli na
kusema kuwa maana ya kuwa na elimu ya juu ni kuonyesha ufanisi.
Naye
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Injinia Brig Gen. Reginald Chonjo ambaye
alimwakilisha Mwenyekiti wa Bodi hiyo alisema kuwa pamoja na kutolewa
kwa vifaa hivyo lakini mafunzo ya namna ya kutumia vifaa hivyo ni muhimu
kuzingatiwa ili vifaa hivyo viweze kufanyakazi zilizokusidiwa kwa
ufanisi na kwa muda mrefu.
Awali
wakati akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Mtendaji Mkuu wa TEMESA Injina
Marcellin Magesa alimshukuru Waziri wa Ujenzi kwa kuweza kutoa
kipaumbele kwa Taasisi hiyo na kuitengea fedha zilizowezesha kupatikana
kwa vifaa hivyo katika kipindi hiki muafaka kwani karakara nyingi tayari
zilikuwa katika hali mbayo kutokana na kukosa vitendeakazi.
0 comments:
Post a Comment