Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto Ummy Mwalimu
akizungumza katika Siku ya Maombi na Matendo kwa Watoto Duniani
iliyoadhimisha jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Don Bosco, Kulia
kwa Waziri ni Naibu Mwakilishi wa UNICEF Paul Edward, Kushoto kwa Waziri
ni Meneja wa GNRC Elizabeth Mwase na mbali kushoto ni Ofisa toka
UNICEF.
.Utafiti umebaini kuwa kati ya watoto 10 watatu wamefanyiwa vitendo vya unyanyasaji
Serikali imekiri kuwa ukatili dhidi ya watoto ni changamoto kubwa kwani utafiti
umebaini kati ya watoto 10 wa kike 3 wameshafanyiwa vitendo vya
unyanyasaji wa kingono na kati ya watoto 7 wa kiume mmoja amesha fanyiwa
vitendo vya unyanyasaji wa kingono au kimwili.
Akizungumza
kwenye Siku ya Maombi na Matendo kwa Watoto Duniani (World Day of
Prayer and Action for Children) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Wanawake na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu amesema vitendo vya unyanyasi wa
kingono na ukatili dhidi ya watoto ni changamoto kubwa kwa serikali,
mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali, jamii, wazazi, walezi na wananchi
kwa ujumla.
“Cha
kushangaza kuwa vitendo vya unyanyasi wa kingono au kimwili na ukatili
dhidi ya watoto vinatendeka mashuleni na majumbani mahali ambapo watoto
wanapaswa kuwa salama,”
“Katika
utafiti huo ilibainika kuwa karibu robo tatu ya wanaume na wanawake
wamewahi kufanyiwa ukatili kabla ya umri wa miaka 18 na watu wazima au
na jamaa zao wa karibu na robo moja wamesababishiwa na mtu mzima ukatili
wa kifkra,” amesema Ummy Mwalimu.
Naibu
Waziri Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto Mhe Ummy Mwalimu
akizungumza na watoto wa shule mbalimbali za msingi na Sekondari.
Amesema
ukatili dhidi ya Watoto na unyanyasaji wa kingono kwa watoto wa kike na
kiume chini ya umri wa miaka 18 una athari kubwa katika siku za baadaye
hasa katika Afya ya jamii husika.
Mwalimu
aliendelea kusema kuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto
imefungua kituo cha pamoja (One Stop Centre) katika hospitali ya amana
jijini Dar es Salaam katika harakati za kusaidia waathirika wa vitendo
vya kikatili na kingono.
Amesema
serikali ya awamu ya nne inajipanga kuja na mkakati mfumo bora zaidi wa
kuwalinda watoto wa kike na kiume dhidi ya vitendo vya unyanyasi wa
kijinsia na ukatili dhidi yao.
Kwa
Upande Meneja Mradi wa Mtandao wa Watoto na Vijana kutoka Imani
Mbalimbali (GNRC) Bi, Elizabeth Mwase amesema pamoja na serikali
kupitisha sheria ya kumlinda mtoto ya mwaka 2009 bado vitendo vya
ukatili dhidi ya watoto vinaongezeka.
Mwase
amesema kuwa asasi za kiraia kwa kushirikiana na serikali wataendelea
kuelimisha jamii umuhimu wa kuheshimu haki za watoto na kuboresha au
kutunga sheria zinazomlinda mtoto mahali popote pale katika makuzi yake.
“jamii
iliyolelewa katika mazingira mazuri ina nafasi kubwa ya kuleta matokeo
chanya kwenye mustakabali wa taifa kwa ujumla lakini jamii iliyolelewa
vibaya haiwezi kubadilisha taifa kwa sababu ni zao la tunda baya,”
amesema.
Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja la Mataifa la Watoto (UNICEF) Paul Edward akisoma risala kwenye Siku ya Maombi na Matendo kwa Watoto Duniani iliyoadhimisha leo jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Don Bosco.
Kwa
upande wake Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja la Mataifa la Watoto
(UNICEF) Paul Edward amesema mwaka 1989 Umoja wa Mataifa iliweka mkataba
wa siku ya kimataifa ya mtoto ili kutambua na kumlinda mtoto dhidi wa
ukatili wa aina yeyote hapa duniani.
Amesema Umoja wa Mataifa, asasi za kirai na mashirika yote yasiyo ya kiserikali wanapaswa kuisaidia jamii na serikali katika kutokomeza ukatili dhidi ya watoto kwa sababu ni taifa la kesho.
Meneja
Mradi wa GNRC Elizabeth Mwase akitoa neno wakati wa maadhimisho hayo ya
siku ya Maombi na Matendo kwa Watoto Duniani akiwa na baadhi ya wageni
waalikwa meza kuu.
Wanafunzi kutoka shule ya Msingi Kumbukumbu wakisoma risala ya watoto.
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akiteta jambo la Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja la Mataifa la
Watoto (UNICEF) Paul Edward.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo.
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akicheza kwaito na wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment