Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametangaza vita rasmi
na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za magendo kupitia bandari bubu
mkoani Tanga na maofisa wa vyombo vya Serikali waliopo kwenye mtandao
huo.
Dk Mwakyembe aliwataka watambue kuwa, kiama chao
kimefika kwa sababu tayari Serikali inayo majina ya wafanyabiashara na
baadhi ya maofisa wa polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka
ya Bandari (TPA) wanaotumika kufanikisha upitishaji magendo.
Dk Mwakyembe ambaye aliwasili Tanga juzi na
kufanya ziara ya ghafla kutembelea bandari bubu zilizoko mkoani hapa,
alitangaza vita hiyo alipozungumza na maofisa wa TRA, polisi, TPA na
wafanyabiashara.
Alisema baada ya Serikali kudhibiti Bandari ya Dar
es Salaam, wafanyabiashara magwiji wa upitishaji bidhaa za magendo
wamehamishia nguvu zao Tanga.
“Natangaza rasmi vita dhidi ya walio katika
mtandao huo, watambue hatuwezi kuruhusu Bandari ya Tanga, bandari bubu
na mpaka wa Horohoro kuwa gulio la walanguzi, wapitishaji dawa za
kulavya na wahamiaji haramu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment