Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela.
JESHI
la polisi mkoa wa Singida, linawashikilia walimu wawili kwa tuhuma ya
kuvunjisha matihani wa kidato cha nne unaoendelea kufanyika hivi sasa
nchini kote.
Walimu
hao ni walimu wa shule ya sekondari kata ya Nkinto wilaya ya Mkalama
mkoani Singida, ambao ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Monica Sebastian
(30) na mwalimu Agaloslo Otieno (32).
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa
Singida, ACP Geofrey Kamwela, amesema kuwa tukio hilo limetokea novemba
13 mwaka huu kati ya saa tatu na tatu usiku katika shule ya sekondari
ya Nkinto kata ya Mwangeza tarafa ya Kirumi wilaya ya Mkalama.
Amesema
kuwa mwalimu Agaloslo akiwa anasimamia mtihani katika shule ya
sekondari ya Mwangeza, alikuwa anaandika baadhi ya maswali ya masomo ya
Kiswahili na Civics kwenye simu yake ya kingajani na kumtumia mwalimu
wake mkuu Monica akiwa shuleni kwake Nkinto.
Kamwela
alisema baada ya Monica kupata maswali hayo,alikuwa anayatafutia majibu
akiwa chooni na wanafunzi walikuwa wanamfuata huko huko chooni kupewa
majibu hayo.
“Lengo
lao ilikuwa ni kuwasaidia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika
mtihani wao wa kidato cha nne mwaka huu.Wanafunzi wenywe waliisha ambiwa
kuwa wawe wanadanganya kwamba wanaenda kujisadia chooni,ili wakapatiwe
majibu na mwalimu mkuu”,alifafanua kamanda na kuongeza;
“Uchunguzi
wa awali wa polisi unaonyesha kuwa uvunjishaji huo ulifanyika kwa
nyakati tofauti kati ya mwalimu mkuu Monica na mwalimu wake Agaloslo
akiwa ana simamia mtihani huo katika shule nyingi.Baada ya mwali mkuu
kutumiwa maswali alikuwa anajificha ndani ya choo cha shule yake na
watahiniwa kwa nyakati tofauti huomba ruhusa kwa wasimamizi kwenda
chooni kwa nia ya kujisaidia na hapo humkuta mwalimu mkuu huyo na kuwapa
maelekezo ya namna ya kujibu maswali hayo”.
Amesema
baada ya Polisi kupata taarifa ya siri kutoka kwa wasamaria wema,
waliweka mtego katika shule ya sekondari ya Nkinto na kufanikiwa
kumkamata mwalimu Monica huku simu yake ikiwa na baadhi ya maswali ya
mtihani.
Alisema
kwa sasa bado wanaendelea na upelelezi zaidi na mara
utakapomalizika,watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
inayowakabili.
0 comments:
Post a Comment