Kamanda wa Kikosi cha
Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua magunia yaliyokuwa na
Pembe za Ndovu yaliokamatwa katika bandari hiyo leo yakiwa katika harakati ya
kusafirishwa nje ya nchi kupitia bandari hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi
la Polisi Bandari Kikosi cha KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40.
Polisi nchini Tanzania wamekamata vipande elfu moja na ishirini na moja vya meno ya tembo vyenye uzito wa karibu kilo elfu tatu.
Meno hayo ya tembo yamekamatwa katika bandari ya
Zanzibar jana na watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na
meno hayo. Hata hivyo, bado haijafahamika idadi kamili ya tembo
waliouawa, kwani baadhi ya meno yamekatwa vipande.Polisi nchini Tanzania wamekamata vipande elfu moja na ishirini na moja vya meno ya tembo vyenye uzito wa karibu kilo elfu tatu.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisema meno hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika kontena la futi arobaini yakiwa yamechanganywa katika mifuko iliyohifadhi makombe ya konokono wa baharini, tayari kwa kusafirishwa nje.
Hivi karibuni raia watatu wa China walikamatwa nchini Tanzania kwa kukutwa na meno 706 ya tembo, sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi mbalimbali nchini humo.
Kukamatwa kwa meno haya ya tembo, kumekuja wakati tayari serikali imetangaza kusitisha Operesheni Tokomeza Ujangili, ambayo ililenga kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka kutokana na kuuawa katika hifadhi za taifa nchini Tanzania. Wanyama wanaolengwa zaidi na majangili kutokana na meno yao na pembe ni tembo na faru.
Magunia haya yakiwa na
shehena na makombe ya Pwani wakati katikati yakiwa na viroba vya Pembe za Ndovu
ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika Kontena likiwa tayari kusafirishwa nje ya
Nchi, limegunduliwa katika bandari ya Zanzibar leo asubuhi
Baadhi ya Pembe za Ndovu
zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar yakisubiri kuhesabiwa kupata
idadi kamili, thamani yake na uzito kwa ujumla.
Operesheni ya kuhesabu Pembe za Ndovu zilizokamatwa katika bandari
ya Zanzibar ikiendelea.
Matukio ya kukamatwa kwa meno ya tembo kutoka Afrika Mashariki yamekuwa yakiripotiwa kila mara. Oktoba, 20, 2012, tani nne za meno ya tembo yenye thamani ya dola milioni 3.4 za Kimarekani yalikamatwa Hong Kong, yakidaiwa kusafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.
Pia Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18 sawa na dola zaidi ya elfu 11, yakisafirishwa kwenda nje.
0 comments:
Post a Comment