Mwasisi wa Chadema,Edwin Mtei amesema kuna baadhi ya watu nchini
wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanafanya njama za kukidhoofisha
na hata kukipoteza kabisa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka
2015.
Mtei,alitoa kauli hiyo wakati chama hicho kikiwa
katika wakati mgumu baada ya baadhi ya viongozi wake kushambuliana
kupitia mitandao ya kijamii, huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani
Arusha,Samson Mwigamba akisimamishwa kwa madai ya kukiuka kanuni za
chama hicho.
Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema kuna baadhi
ya watu kutoka Chama Tawala cha CCM wanahakikisha wanatengeneza
mifarakano kila kukicha ili kukivuruga Chadema.
Alisema mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa
kauli kuwa huenda CCM ikang”oka mwaka 2015, baadhi ya makada na viongozi
wameanza kukesha wakifanya mbinu ya kukivuruga ili Chadema kisishike
dola.
“Kuna watu wa CCM wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanatuvuruga, ili tusishike dola mimi nasema hawatuwezi”alisema Mtei
Hatahivyo,alisema kitendo cha kusimamishwa na hata
kufukuzwa baadhi ya makada wa Chadema kimetokana na usaliti ndani ya
chama hicho huku wengine wakikubali kutumiwa na CCM.
0 comments:
Post a Comment