Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya Strabag wamegoma na kusimamisha shughuli zote za kampuni hiyo kwa saa tisa, kutokana na agizo la kuhamishiwa kwa mwajiri mwingine.
Vibarua hao zaidi ya 160 wanaojenga barabara za
mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam, kwa kushirikiana na wafanyakazi
waliojiriwa waligoma na kufunga lango kuu la kuingia ofisi za kampuni
hiyo zilizopo Ubungo.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wafanyakazi
hao wakiwa katika makundi nje ya lango kuu la kampuni hiyo, huku magari
kadhaa yakiwa yamepanga foleni kusubiri kuingia kushusha vifaa.
Wafanyakazi hao walisema wamefikia hatua hiyo
kutokana na taarifa za Kampuni ya Raba kuchukua dhamana ya kuwasimamia
vibarua wote, hivyo hakutakuwapo na mkataba mwingine kati yao na
Strabag. Walisema hatua hiyo ambayo inaonekana kufanyika bila kuzingatia
sheria, kwani walipaswa kulipwa haki zao kabla ya kuhamishiwa kampuni
nyingine.
Licha ya madai hayo, wafanyakazi hao walionekana
kulalamikia ujira mdogo wanaolipwa na Kampuni ya Raba, ikilinganishwa
na kiwango walichokuwa wakilipwa na Strabag.
Walisema awali walikuwa wakilipwa Sh17,000 kwa
siku, lakini baada ya kuhamishwa malipo yameshuka hadi Sh10,000 ambazo
hakiwawezeshi kukidhi mahitaji.
Kufuatia mgomo huo, kuchukua saa kadhaa, Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana aliwasili eneo kuwasikiliza
wafanyakazi hao na kupata suluhu.
Rugimbana aliwataka wafanyakazi na vibarua hao wakutane leo kwa ajili ya kutafuta mwafaka.
0 comments:
Post a Comment