
Jaji
wa Mahakama Kuu Zanzibar Abdulhakim Ameir Issa akifungua warsha kuhusu
udhibiti wa Utakasishaji wa Fedha haramu katika Hoteli ya Visitors Inn
Jambiani. Kushoto ni Kaimu Kamishna Kitengo cha Udhibiti wa Fedha
haramu Tanzania Onesmo Hamis Makombe na kulia ni Msaidizi mambo ya
Utawala wa kitengo hicho Jamila Lutanjuka.

Kaimu
Kamishna Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu Tanzania Onesmo Hamis
Makombe akimkaribisha Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Abdulhakim Ameir
Issa kufungua warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa Fedha haramu kwa
wadau mbali mbali katika Hoteli ya Visitors Inn Jambiani Mkoa wa Kusini
Unguja.

Washiriki
wa warsha kuhusu udhibiti wa Utakasishaji wa Fedha haramu
wakimsikiliza Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Abdulhakim Ameir Issa wakati
akifungua warsha hiyo inayofanyika Hoteli ya Visitors Inn Jambiani Mkoa
wa Kusini Unguja.

Picha
ya pamoja ya washiriki wa warsha kuhusu udhibiti wa Utakasishaji wa
Fedha haramu inayofanyika Hoteli ya Visitors Inn Jambiani Mkoa wa Kusini
Unguja.(Picha na Ramadhani Ali wa Maelezo Zanzibar).
SERIKALI
itaendelea na jitihada za kuhakikisha kua mapambano dhidi ya
utakasishaji wa fedha haramu yanaendelea ili kulinusuru Taifa na
madhara ya kiuchumi, kisiasa ,kiusalama na kijamii na athari za
Kimataifa .
Hayo
yameelezwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu katika hotuba
ya ufunguzi wa warsha ya udhibiti wa fedha haramu iliyosomwa kwa niaba
yake na Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Abdulhakim Ameir Issa katika
Hoteli ya Visitors Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema
Serikali imetunga sheria ya udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu ya
mwaka 2006 na sheria ya udhibiti utakasishaji wa fedha haramu na mali
athirika ya Zanzibar ya mwka 2010 fedha ambazo hupatikana kwa njia ya
haramu kitendo ambacho huwa ni kosa la jinai pande zote mbili za
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Utakasishaji
wa fedha haramu lipo kwa kua vitendo vya kihalifu vinavyowapatia pato
haramu wahalifu hao kama Biashara ya dawa za kulevya,Rushwa, ujangili,
ujambazi pamoja na ukwepaji wa kodi na uharamia haya yote hupelekea
kuwepo kwa fedha haramu hivyo Serikali inafanya jitihada kubwa ya
kupambana na wahalifu hao”, alisema Jaji Abdulhaki Ameir Issa.
Kaimu
Kamishna wa Kitengo cha Udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu
Tanzania Onesmo Hamis Makombe ametoa wito kwa Taasisi za Serikali,
taasisi binafsi na wananchi kwa jumla kushirikiana ili kupambana na
uhalifu huo unaofanywa na watakasishaji wa Fedha haramu.
Amesema vitendo vya utakasishaji wa fedha haramu vinaishushia hadhi nchi na kupelekea kudharauliwa na Jumuia za Kimataifa.
“Katika
kupambana na vitendo hivyo kumeundwa vitengo vya kanda katika nchi
mbali mbali duniani na Jumuia ya Kimataifa inatoa kila msaada kuviunga
mkono vitengo hivyo”, alisema Onesmo Hamis Makombe.
Mshiriki
wa warsha hiyo kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar Walid
Mohd Adam amesema dhana ya udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu ni
mpya kwa wananchi waliowengi hivyo elimu zaidi inafaa kutolewa kwa
wananchi.
Amesema
watu wengi hujipatia fedha kwa njia zisizo halali na hatimae hufanya
mipango ya kuzisafisha ili zionekane halali na kuiweka nchi katika hali
mbaya kiuchumi, kibiashara na kupoteza heshma machoni mwa Jumia ya
Kimataifa.
0 comments:
Post a Comment