Naibu
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kulia) akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu mkutano wa kupitia utekelezaji wa Bajeti Kuu ya
Serikali (GBS) ulioshirikisha na Washirika wa Maendeleo(DPS) na wadau
mbalimbali kutoka serikalini uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa
Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu
wa wizara hiyo Profesa Adolph Mkenda.
Mwenyekiti wa
Washirika wa Maendeleo Balozi wa Sweden , Lennarth Hjeimaker (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa
kupitia utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS)
ulioshirikisha na Washirika wa Maendeleo(DPS) na wadau mbalimbali
kutoka serikalini uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.
Nyerere jijini Dares Salaam (kulia) Naibu Waziri wa Fedha Saada
Mkuya Salum .
Serikali
imesema kwamba itaendelea kuelekeza rasilimali katika
masuala ya elimu, afya, kilimo ikiwa ni hatua ya kuweza kupunguza
umasikini kwa haraka ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto
zilizopo katika sekta mbalimbali .
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkutano
wa mwaka 2013 wa kupitia utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS)
ulioshirikisha na Washirika wa Maendeleo(DPs) na wadau mbalimbali
kutoka serikalini uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.
Nyerere jijini Dares Salaam.
“Changamoto
inayotukabili ni kuleta maendeleo kwa haraka. Uchumi wa nchi unakuwa
kwa asilimia 7 lakini umasikini umepungua kwa asilimia 2,”alisema Waziri
huyo.
Alisema changamoto
inayoikabili serikali ili kukabiliana na umasikini nchini ni
kuhakikisha inaelekeza rasilimali zake ili ziweze kuzalisha ajira
.Pia kuangalia idadi ya watu kulingana na uchumi wa nchi.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri huyo kufuatia Mwenyekiti wa
Washirika wa Maendeleo Balozi wa Sweden ,
Lennarth Hjeimaker kueleza kuwa hatua za kupunguza umasikini na
upatikanaji wa huduma za jamii bado ni ndogo ,kiwango cha ufaulu kwa
shule za sekondari na msingi kushuka na uwiano wa walimu na wanafunzi
bado mdogo, zaidi ya nusu ya watu vijijini wahapati maji safi na salama
na upatikanaji wa nishati vijijini bado ni changamoto.
Wadau hao pia wameishauri Serikali kuendelea kupambana na tatizo la rushwa nchini.
Katika
kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2012/2013 wadau hao walichangia
Dola za Marekani milioni 560 na mwaka huu wa fedha waliahidi kutoa Dola
za Marekani milioni 561 hivyo hadi sasa Serikali imeshapokea Dola za
Marekani milioni 290.2.
0 comments:
Post a Comment