Naibu mkuu wa usalama wa taifa
nchini Libya, Mustafa Noah, ameachiliwa huru siku moja baada ya kutekwa
na watu wasiojulikana wakiwa na silaha karibu na uwanja wa ndege wa
Tripoli.
Wakati akitekwa hakuwa na walinzi wake.Mapigano hayo yaliwahusisha wanamgambo na waandamanaji, ambao walikuwa wakijaribu kuwafukuza wanamgambo kutoka mji mkuu Tripoli.
Serikali imekuwa ikijitahidi kuwafukuza wanamgambo hao.
Mgomo wa kutaka wanamgambo waondolewe kutoka Tripoli, umedumu kwa siku tatu.
Waziri Mkuu, Ali Zeidan, alitekwa nyara kwa muda mfupi mwezi uliopita.
0 comments:
Post a Comment