Katibu
Mkuu wa Zanzibar Association for Youth, Education and Empowerment,
Fatma Mabrouk Khamis akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina
hiyo ya ujasiriamali wa kuandika michanganuo ya kuandika biashara.
Watanzania
wameombwa kuwa na utamaduni wa kujitokeza kwa wingi katika semina
mbalimbali zinazolenga kuhamasisha na kufundisha ujasiriamali katika
harakati za kupambana na tatizo la ajira nchini. MOblog inaripoti.
Akizungumza
na Moblog jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa
Zanzibar Association for Youth, Education and Empowerment, Fatma Mabrouk
khamis amesema wao Jumuiya ya wanawake wa wajasirimali Tanzania kwa
kushirikiana na taasisi ya Kinu waliandaa semina ya mbili ya jinsi ya
kufundisha kuandika michanganuo ya kibiashara kwa wajasiriamali vijana
nchini.
“Tumepata
takribani vijana kumi na moja toka sehemu mbalimbali za mkoa wa Dar es
Salaam na wamefundishwa jinsi ya kuandika michanganuo ya kibiashara na
kuanza biashara kwa mtaji wa chini,” amesema Fatma.
Amesema
kuwa washiriki wa semina walikuja na mawazo ya kuanzisha biashara
mbalimbali kama kuhamasisha utalii wa ndani, biashara kwa mfumo wa
teknonojia, biashara za kimataifa na kurasa zinaonyesha uainisho wa
biashara na makampuni mbalimbali.
Bi.
Khamis amesema kuwa katika Ujasiriamali kuna mbinu nyingi za kuweza
kumfanya mjasiriamali kuweza kujitanua na kufanya biashara za ndani za
kikanda na kimataifa endapo watakuwa wabunifu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Professional Approach Development
(PAD) Lilian Secelela Madeje amesema kuwa kikundi chao kwa ksuhirikiana
na taasisi ya kinu watashirikiana na taasisi za fedha kuelezea
changamoto za upatikanaji wa mitaji katika kuanzisha biashara.
Madeje
alisisitiza kuwa mjasiriamali unaanzia kwenye wazo ambalo baadaye
linakuwa kwenye vitendo kupitia taasisi za fedha zenye kutoa mikopo kwa
riba nafuu katika kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo wa watanzania.
Lilian
Secelela Madeje Mkurugenzi Mtendaji wa Professional Approach
Development akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo ya Wajasiriamali.
Wajasirimali wakiwa katika vikundi wakiandaa michanganuo ya biashara mbalimbali wakati wa kipindi cha majaribio.
0 comments:
Post a Comment