Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jinsi ya
kutumia vifaa vya maabara katika kufanikisha kutambua kemikali kutoka
kwa wanafunzi wa kidato cha nne Erasto Ndumba na Stella Hyera wa shule
ya sekondari ya Kata ya Mtakatifu Paul kata ya Liuli wilaya ya Nyasa
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi nyumba za
madaktari zilizochini ya mradi wa Taasisi Benjamini Mkapa katika kituo
cha afya Mkili kata Liundi wilayani Nyasa.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishauri jambo kabla ya kuvuka
mtu Ruhuhu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na
Mwenyekiti wa CCM Ndugu Oddo Mwisho.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na Mkuu
wa Wilaya ya Nyasa Ndugu Ernest Kahindi wakivuka kwa mtumbwi kuelekea
kijiji cha Kipingu wilaya ya Ludewa.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu
wakazi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa, Kijiji hicho kipo mpakani
wa mkoa wa Ruvuma na Njombe.
Katibu
Mkuu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata
Kipingu kijiji cha Kipingu wilaya ya Ludewa ambapo aliwaambia ahadi ya
kujengwa kwa daraja la mto Ruhuhu, uzalishaji wa umeme utakotosheleza
mahitaji ya wilaya ya Nyasa na Ludewa pamoja na mradi wa umwagiliaji.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia wananchi wakati akirejea
kijiji cha Lituhi kwa Mtumbwi baada ya kutoka kuwasalimu wakazi wa
kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa,wengine pichani ni Dk.Asha-Rose
Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa pamoja na Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na kikundi cha akina
mama wakulima wa mpunga na mboga mboga wa kijiji cha Lituhi katika
viwanja vya Lituhi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Verena Shumbusho
wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba
wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mikutano
Lituhi ambapo vijana 12 kutoka vijiji mbali mbali walipewa mabati kwa
ajili ya kuezeka nyumba zao.
Mbunge
wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akimtambulisha Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kama Ndugu yake wa karibu kwani mafanikio
yake yametokana na mchango mkubwa wa Marehemu Mzee Nnauye ,Pia Komba
alimuelezea Kinana kama mmoja wa walimu wake wazuri wa masomo ya kijeshi
pamoja na siasa.
0 comments:
Post a Comment