Welcome to our online store Portal

Template Information

Saturday, November 23, 2013

AKINA MAMA 19 NA WATOTO 137 WAFARIKI KILA SIKU

Meneja Mradi wa 'Wajibika Mama Aishi', David Lyamuya akiwasilisha mada katika semina ya wahariri na waandishi wa habari iliyofanyika Regency  Hotel jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi wa ‘Wajibika Mama Aishi’, David Lyamuya akiwasilisha mada katika semina ya wahariri na waandishi wa habari iliyofanyika Regency  Hotel jijini Dar es Salaam.
Rais wa UTPC, Kenny Simbaya akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Rais wa UTPC, Kenny Simbaya akiwasilisha mada kwenye semina hiyo.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakihudhuria semina hiyo
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakihudhuria semina hiyo.
IMG_0002
Washiriki wa semina pamoja na wawezeshaji.
Washiriki wa semina pamoja na wawezeshaji.
JUMLA ya watoto 137 na wajawazito 19 hufariki dunia kila siku nchini Tanzania kwa matatizo yanayotokana na uzazi. Vifo vya watoto pekee wanaopoteza maisha kutokana na matatizo hayo kwa mwaka hufikia 50,000 kwa nchi nzima.
Takwimu hizi za kusikitisha zimetolewa jijini Dar es Salaam na Meneja Mradi wa mpango wa ‘Wajibika Mama Aishi’, Bw. David Lyamuya toka Taasisi ya Utepe Mweupe katika semina ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi.

Lyamuya alisema mbali na idadi hiyo kubwa ya akinamama pamoja na watoto kupoteza maisha yapo matukio mengine ya vifo ambayo hayaingizwi kwenye takwimu, hali inayoonesha huenda vifo hivyo ni zaidi ya takwimu halisi zilizopo.
Alisema kuna kila sababu kwa mamlaka husika kwa kushirikiana na jamii kulivalia njuga suala hilo ili kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinakoma. Aidha alisema licha ya uhimizaji wa wajawazito kuhudhuria klini bado idadi kubwa hasa vijijini wanajifungulia nyumbani kutokana na umbali mrefu wa sehemu zinapotolewa huduma za afya.
“…Sisi tumefanya utafiti katika Mkoa wa Rukwa kuangalia hali ya upatikanaji huduma za afya kwa wajawazito. Yapo maeneo mama aliyefikia hatua ya kujifungua (mwenye uchungu) hutakiwa atembee kilomita 94.5 ndiyo anakutana na kituo cha afya, sasa mtu aliye na hali kama hiyo hawezi kutembea umbali mkubwa kiasi hicho hivyo hulazimika kujifungua nyumbani,” alisema Lyamuya.

Aidha aliongeza kuwa taasisi ya Utepe Mweupe (The White Ribbon Alliance) kwa sasa inaendesha kampeni ya miaka mitatu ya “Wajibika Mama Aishi” ikiwa ni moja ya hatua ya kushawishi kila mmoja kuwajibika kuhakikisha anakabiliana na vifo vya akinamama na watoto vinavyotokea hasa wakati wa kujifungua.
Hata hivyo aliwataka wanahabari kuhakikisha wanatumia nafasi zao kutoa mchango wa kuvishavishi vyombo husika na wanajamii kwa ujumla kupambana na vifo vya akinamama na mtoto.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop