ZITTO, DR. KITILA MKUMBO NA SAMSON MWIGAMBA WAVULIWA UONGOZI CHADEMA, SAID AMOUR ARFI AJIUZULU
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemvua nyadhifa zote Naibu Katibu
mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini. Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama
hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama kwa
kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha
chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake. Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi
wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na
mwingine mmoja Makao makuu wamepewa siku kumi na nne wajieleze
kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwemo
kuvuliwa Uanachama.
Wakati hayo yakiendelea naye Makamu
Mwenyekiti wa Chama hicho Bara na Mbunge wa Mpanda Said Amour Arfi
ameamua kuandika waraka wa kujizulu wadhifa wake kama ifuatavyo;
Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara
kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani
ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na
wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia,
hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.
Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano
yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda
na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua
maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo
mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni
Unafiki wa kupindukia.
Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei
kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na
utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla
kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika
maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu
Nawasilisha.
Said A Arfi (mb)
Related Product :
Why Shop on Bongo Online?
We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be
0 comments:
Post a Comment