Monday, November 25, 2013

WAZIRI NCHIMBI ATEMBELEA ZAMBIA ZIARA YA KIKAZI

  PIX 1-ZAMBIA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akibadilishana mawazo  na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Zambia, Edgar Lungu, ofisini kwake jijini Lusaka nchini Zambia. Waziri Nchimbi yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ambapo katika majadiliano yao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo kwa kuboresha huduma katika Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Idara ya Wakimbizi ili yaweze kutoa huduma nzuri zaidi kwa wananchi.. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 2-ZAMBIA
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma (kushoto) akifuatilia kwa makini majadiliano kati ya Waziri ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kulia) na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Zambia, Edgar Lungu (hayupo pichani). Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Lungu, jijini Lusaka nchini Zambia. Waziri Nchimbi yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya wizara hizo kwa kuboresha huduma katika Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Idara ya Wakimbizi ili yaweze kutoa huduma nzuri zaidi kwa wananchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 3-ZAMBIA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimsikilza kwa makini mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Zambia, Edgar Lungu, ofisni kwake jijini Lusaka nchini Zambia wakati walipokuwa wanajadiliana masuala mbalimbali yaliyopo ndani ya wizara zao. Waziri Nchimbi yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ambapo wamekubaliana na Waziri Lungu kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo kwa kuboresha huduma katika Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Idara ya Wakimbizi ili yaweze kutoa huduma nzuri zaidi kwa wananchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About