Friday, December 13, 2013

AJALI MBAYA YA BASI YATOKEA MKOANI TANGA,12 WAFARIKI PAPO HAPO


Basi la Abiria la Kampuni ya Burudani linavyoonekana baada ya kupata ajali mbaya sana leo iliyopelekea kupoteza maisha kwa watu 12 huku wengine zaidi ya 30 wakiwa kwenye hali mbaya.ajali hiyo imetokea leo eneo la Kwaluguru,Kwedizinga  wilayani Handeni,Mkoani Tanga.
Watu 12 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada  ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Burudani linalofanya safari zake kati ya Korogwe mkoani Tanga kwenda Jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

 Ajali hiyo imetokea mapema leo asubuhi majira ya saa 1.30 katika eneo la Kwaluguru,Kwedizinga  wilayani Handeni,Mkoani Tanga.
Akithibitisha kutokea ajali hiyo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga,Constantine Massawe alisema kuwa ajali hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili T 610 ATR aina ya Nissan,imetokea leo na kusababisha vifo vya abiria 12 na wengine zaidi ya 30 wako kwenye hospitali ya Wilaya ya Korogwe,wakiendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda Massawe aliendelea kusema kuwa  dereva wa basi hilo ajulikanaye kwa jina la Luta Mpenda(35) ni miongoni mwa watu wanaosadikiwa kufa na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Korogwe ya Magunga.

“Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya magunga na hali zao bado siyo nzuri sana lakini na miili ya marehemu pia imehifadhiwa magunga”,alisema Kamanda Massawe.
Hata hivyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo alipofika kwenye kona ya eneo la Kwalaguru gari lilimshinda na  kupinduka. 
Wakazi wa Wilaya ya Korogwe wakiwa wamefurika kwenye Hospitali ya Magunga walipohifadhiwa marehemu na majeruhi.
Wauguzi wa Hospitali ya Magunga wakiendelea kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo akitokea chumba cha maiti cha Hospitali hiyo.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About