IMG_7030
MKurugenzi wa Kampuni ya Blue Sky, Richard Signeski (kulia), akizungumza  na waandishi wa habari (hawapo pichani), katika ukumbi Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam  kuhusu ushirkiano walioingia na  Kampuni ya Status Communications ya nchini kuwawezesha waandaaji filamu nchini kuuza filamu zao  kwenye mitandao ya kijamii. Kushoto ni Mwakilishi wa Status Communication, Monalisa Shayo.
IMG_7022
Omar Salisbury akizungumza na waandishi wa habari.

Kampuni ya Status Communications leo imetangaza ushirikiano na kampuni ya usambazaji wa filamu ya Kimarekani Blue Sky Media ili kuwawezesha kuuza filamu kwenye mitandao ya ITunes, Microsoft, You Tube, RAIN na mitandao mingine ya kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Blue Sky, Richard Signeski alisema ushirikiano huu utawafanya watengeneza filamu kutoka Afrika Mashaaiki na kati kuweza kuuza filamu moja kwa moja kwenye mitandao mikubwa ya usambaji dunia nzima.

‘’Lengo la ushirikiano huu ni kuwapa watengeneza filamu kutoka Afrika mashariki na kati kuweza kuuza filamu zao moja kwa moja kwa watazamaji dunia nzima’’ alisema Signeski.
Mwakilishi wa Status Communications, Monalisa Shayo alisema ushirikiano wao na Blue Sky ni moja ya tu ya ushirikano na makampuni ya kimataifa wanaotaka kuingia katika soko la Afrika Mashariki.
 ‘’Mwaka 2013 umekuwa mwaka muhimu kwa Status Communications kwani tumeweza kuingia mikataba na makampuni mbalimbali ili kuweza kuingia soko la Afrika Mashariki’’ alisema Monalisa.
‘’Mwanzoni mwa mwaka huu tumeingia mikataba na makampuni kama Media Zone Authority  ya Abu Dhabi (twofour54) pamoja na Qatar’s Media Group International pamoja na Visual Unity ya Abu Dhabi ili kuwawakilisha kwenye masoko yao kwenye miji kama ya Prague’ alisisitiza Monalisa wa Status Communications.

‘’Fursa hii ni muhimu kwa watengeneza filamu wa Afrika Mashariki kuuza filamu kwenye masoko tofauti duniani’’ alisema Monalisa.
Akielezea sababu za kuja nchini, Signeski alisema alichokigundua hapa nchini ni kuwa watengeneza filamu wengi wanahofia kuwekeza fedha nyingi kwenye utengenezaji wa filamu zao kwani wanahofia uchache wamasoko ya kuuza filamu zao.
‘’Hivyo nawaomba watengeneza filamu mjitokeze kwa wingi ili muweze kuuza filamu dunia nzima kwa urahisi’’ alimaliza Signeski.