Wednesday, December 4, 2013

Singapore imekubali kubadilisha Mji wa Lindi kua mji wa Kimataifa

http://www.azizicompdoc.blogspot.com/
Serikali imesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na nchi ya Singapore kwa ajili ya uboreshaji mipango miji Lindi,Mtwara,Dar es Salaam na Arusha
Akizungumza baada ya utiaji saini huo jana, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Kidala alitolea mfano wa Dar es Salaam kuwa, tangu miaka ya 1990 mpango wa uboreshaji jiji haujabadilishwa.
“Kutokana na mkataba huu, sasa mpango wa uboreshaji Jiji la Dar es Salaam na majiji mengine utapitiwa na kufanyiwa marekebisho yanayoendana na wakati huu,” alisema Kidala na kuongeza;
“Kuna kampuni kutoka nchini Italia ambayo imeandaa uboreshaji huo, utapitiwa na Shirika la Upangaji Miji la Singapore kabla ya kuanza utekelezaji.”
Alisema mkataba huo umelenga maeneo matatu ambayo ni; uboreshaji mipango miji, ushirikiano wa ujenzi nyumba za gharama nafuu na kujenga mfumo mzuri wa kumiliki ardhi.
Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye alisema makubaliano hayo yametokana na ziara iliyofanywa hivi karibuni nchini Singapore na Rais Jakaya Kikwete na wabunge wa Kamati ya Bunge ya Bajeti na Hesabu za Serikali (PAC).
“Mikoa ya Lindi na Mtwara kuna shughuli za uchumbaji gesi, hivyo ni muhimu kuhakikisha uendelezaji majengo na miundombinu ya eneo hilo inakuwa ya kisasa,” alisema Medeye na kuongeza:
“Baadaye mpango huu utaendelea Mbeya, Mwanza na Tanga. Singapore wamepiga hatua katika suala la uendelezaji miji, wana uzoefu wa kutosha hivyo tunaamini watatusaidia.”
Alisema mpango huo umeanza rasmi jana kwa wataalamu wa Tanzania kukutana na wale wa Singapore, kujadiliana mambo ambayo wataanza kuyatekeleza katika mikoa na majiji hayo.
“Kuna masuala ya ardhi, nyumba na mengine mengi, kila eneo lina wataalamu wake, kazi hii inaanza mara moja na itakuwa ni ya miaka mitano,” alisema.
Mwenyekiti wa Shirika la Upangaji Miji la Singapore, Seah Moon Ming alisema njia nzuri ya kuendeleza miji, ni kuwa na mipango thabiti ya ujenzi mzuri wa nyumba na miundombinu.
Ming alisema licha ya kuendeleza miji, nchi yake imetoa wataalamu ambao watashirikiana na wenyeji lengo likiwa ni kupiga hatua kwenye maendeleo haraka, kwa wananchi kumudu gharama za nyumba nafuu.
Quantity : Add to Cart

1 comment:

Labels

Blogroll

Labels

About