Sekta
ya mawasiliano ya simu Tanzania na Afrika Mashariki leo imepata
matumaini mapya kufuatia kuingia kwa kampuni mpya ya simu ya kipekee, ya
ubunifu, kwa jamii, na yenye ushindani kuliko zote, kuzinduliwa
bila jina.
Pamoja
na ahadi yake ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mawasiliano ya mtandao
wa simu, kampuni hiyo mpya kwa wakati mmoja imezindua pia kampeni ya
kiubunifu inayotambulika kwa jina la “Tupe Jina” itakayofanyika kwa njia
ya mtandao na ujumbe mfupi katika simu kwa lengo la kuipa fursa Afrika
Mashariki kuichagulia jina bora kampuni hii kwa kupiga kura.
Hii
ni kampuni ya kwanza ya simu Afrika Mashariki ambayo kweli inajali na
haigopi kuamini watu, na hakuna kampuni nyingine inaweza kuthubutu
kufanya hivyo. Hakuna kampuni yoyote duniani iliyoweza kuzinduliwa bila
jina na kutoa jukwaa kwa kampeni ya kusisimua ya siku 10 kabla ya jina
kuwekwa hadharani.
“Tupe
Jina” ni kampeni itakayoanza Novemba 25, 2013 hadi 4 Desemba 2013 kwa
awamu mbili katika mtandao, ujumbe wa simu na mtandao wa kijamii wa
facebook. Katika awamu ya kwanza, Afrika Mashariki inapaswa kuteua
majina ambayo wanapenda hii kampuni mpya iitwe.
Mshirki anaweza kuchagua jina kwa kuingia katika mtandao wa Unaweza kuteua jina kwa njia ya magogo kwenye mtandao wa www.giveusaname.net au kutuma ujumbe wa simu ukiambatanishwa na jina analopendekeza kwenda namba 15678 au aingie katika mtandao wa www.facebook.com/giveusaname.
Katika awamu ya pili ya kampeni, jopo litatathmini majina yote na
itatoa majina matano ambayo yamependekezwa mara nyingi zaidi, ya kipekee
na yenye ubunifu.
Baada
ya hapo Afrika Mashariki watapiga kura kwa ajili ya kupata jina bora
moja ambalo hatimaye litakuwa jina la kwanza la kampuni hii ya
mawasiliano ya simu ambayo daima itakuwa ya kwanza ya Kiafrika
Mashariki. Mshindi katika kampeni hii, mtu ambaye atakuwa amechagua jina
ambalo hatimaye litakuwa la kampuni atajishindia muda wa bure wa kupiga
simu za ndani na SMS bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Zawadi
zingine zitakuwa simu za kisasa za ‘smartphone’ na kompyuta za
kiganjani (tablets) kwa washiriki wa kampeni hii ya “Tupe Jina”. Kwa
muitikio wa Afrika mpya, balozi wa jina hilo ambaye ni mchekeshaji Bw
Hemedi Khalida “Mkwere” atasherehekewa, ambaye amesimama katika mstari
wake kwa kipindi cha television cha “Mizengwe” ambacho kinapata kasi
kila siku.
Kutokana
na wataalam kutabiri kuongezeka kwa pato la taifa la Tanzania kutoka
asilimia 4 hivi sasa hadi asilimia 7 mwaka 2015, sekta ya mawasiliano
ina nafasi kubwa ya katika ukuaji wa uchumi katika miaka ijayo na
kampuni hii mpya ya mawasiliano ya inawakilisha sura ya kasi hii kubwa
ya ukuaji.
Tanzania
inabaki kuwa ni moja ya nchi zenye kiwango cha kuingiza simu chini ya
asilimia 50 kufikia Juni 2013, jumla ya matumizi ya mawasiliano ya simu
nchini humo ni chini ya wastani kwa nchi za Afrika.
Hii
kampuni mpya ya simu kwa umuhimu mkubwa itawekeza kiasi kikubwa cha
fedha kutoka kwa wateja wake kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu kwa
watu wa Uganda katika sekta ya afya na hasa katika tiba za kimtandao na
vituo vya elimu ya masafa.
Hii
tafsiri yake ni kwamba kuwekeza idadi kubwa ya faida katika kuwezesha
Afrika Mpya kuzingatia ongezeko la watumiaji wa mawasiliano ya simu, na
zawadi bora ambayo kampuni hii inatarajia katika miaka ijayo ni kukuza
sekta ya afya.
Kampeni
ya “Tupe Jina” itaisha Desemba 4 baada hapo wananchi wa Tanzania
watapata nafasi ya kupeleka namba zao wanazopendekeza kabla ya
kutangazwa na kuwekwa hadharani kwa jina la kampuni.
0 comments:
Post a Comment