Sunday, December 1, 2013

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Parseko V Kone afunga semina ya siku mbili ya soko la kukuza Ujasiriamali


DSC04629
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone, akifungua semina ya siku mbili iliyohusu soko la kukuza ujasiriamali (EGM) iliyoandaliwa na soko la hisa la Dar-es-salaam (DSE) na kufadhiliwa na Financial s=Sector Deepening trust (FSDT).Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Aque Vitae hotel mjini Singida. Kushoto ni Afisa Mahusiano na mshauri wa masula ya Kisheria wa soko la Hisa  Dar-es-salaam, Bi.Mary Mniwasa na kulia ni mwenyekiti  wa TCCIA mkoa wa Singida,Francis Mashuda.
DSC04620
Baadhi ya wajasiriamali na wafanyabiashara mjini Singida,waliohudhuria semina ya siku mbili iliyohusu soko la kukuza Ujasiriamali (EGM) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aqua Vitae hoteli mjini Singida.
DSC04640
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone (wa pili kushoto) akijadiliana jambo na Afisa Mahusiano na mshauri wa masuala ya Kisheria wa soko la Hisa la Dar-es-salaam,Bi. Mary Mniwasa,(wa pili kulia) muda mfupi baada ya kufungua semina ya siku mbili iliyohusu soko la kukuza Ujasiriamali (EGM).
DSC04635
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone,(wa pili kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali na wafanyabiashara wa mjini Singida waliohudhuria semina ya siku mbili ya soko la kukuza Ujasiriamali (EGM).Wa kwanza kulia (walioketi) ni afisa mahusiano na mshauri wa masuala la kisheria wa soko la hisa la Dar-es-salaam (DSE) Mary Mniwasa na kushoto ni mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Singida,Francis Mashuda.(Picha na Nathaniel Limu).
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About