Monday, December 9, 2013

RIPOTI YA CAG YAWEZA KUWAONDOA MADARAKANI BAADHI YA MAWAZIRI


http://azizicompdoc.blogspot.com/
Kuna kila dalili kuwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na zile za Kamati za Bunge zinazosimamia fedha za umma, huenda zikawang’oa baadhi ya mawaziri.
Hofu kuu inaonekana kuwakumba baadhi ya mawaziri huku waziri mmoja mwandamizi aliyezungumza na gazeti hili akisema; “Wengi wetu tumeshikwa na kihoro, hatujui nini kitatokea.”
Ni ripoti za aina hiyo zilizowasilishwa bungeni Aprili 2012, zilisababisha kuwapo shinikizo kwa Rais Jakaya Kikwete kupangua baraza lake la mawaziri, Mei 4, 2012 na kuwatupa nje mawaziri hao.
Katika panguapangua hiyo, Rais Kikwete aliwatosa mawaziri sita akiwemo Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko na Mbunge wa Moshi Vijijini,Dk Cyril Chami.
Wengine waliotoswa kwa shinikizo hilo la wabunge ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu.
Pia Naibu Waziri wa Uchukuzi wa wakati huo, Athuman Mfutakamba alitoswa sanjari na Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya.
Katika mkutano huu wa 14 unaoendelea, zipo tetesi kuwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamejipanga kuwang’oa mawaziri kamili sita na manaibu mawaziri saba kwa kushindwa kuwajibika.
“Hizi siku nne za taarifa za kamati, inawatia kiwewe baadhi ya mawaziri na hakuna ubishi ripoti hizi zinaweza kuchochea kuwapo uamuzi mgumu,” alidokeza mmoja wa mawaziri waandamizi.
Mbunge wa Ubungo na Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, John Mnyika, alisema pia kila waziri kivuli wa wizara ambayo imeonekana kuongozwa na waziri mzigo, amepewa maelekezo maalumu.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About